Na Tito Mselem, Chunya
Waziri wa Madini Doto Biteko amewasimamisha kazi Maafisa Madini wote wa
Ofisi ya Madini Chunya Mkoani Mbeya na kuteua Wajiolojia watakaokaimu nafasi
hizo wakati wizara ikitafuta Maafisa wengine waaminifu watakaofanya kazi hizo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kugundua wizi mkubwa wa madini ya dhahabu
unaofanywa na maafisa hao wakishilikiana na wamiliki wa kampuni ya uchenjuaji
wa dhahabu.
Akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo wadogo pamoja na
wamiliki wa makampuni ya uchenjuaji wa dhahabu Waziri Biteko, amesema udanganyifu
unaofanywa na Maafisa hao wa Madini pamoja wenye kampuni hizo za uchenjuaji ni mkubwa na hahuitaji msamaha hata kidogo.
“Mimi kama Waziri mwenye dhamana katika sekta hii ya Madini ninawapenda
sana wachimbaji ila nasikitika sana kwa wachimbaji na wenye makampuni ya
uchenjuaji kutokuwa waaminifu,” amesisitiza Waziri Biteko
Ameongeza kuwa, Maafisa wa madini hao ndiyo wanaotoa mianya ya wizi wa
dhahabu unaofanyika kwenye kampuni zaa uchenjuaji wa dhahabu wilayani humo.
Aidha, katika ziara hiyo Biteko ameifunga kampuni ya Ntorah Gold Company Ltd inayohusika na uchenjuaji
wa dhahabu wilayani humo baada ya kutoa
taarifa za udanganyifu kwa serikali.
Pia, Waziri Biteko ameongeza kwamba, Wilaya ya Chunya ndiyo
sehemu pekee Tanzania inayoongoza kwa wizi wa dhahabu na kutoa taarifa za uongo
za kampuni za uchenjuaji wa dhahabu ikifuatiwa na wilaya ya Kahama iliyopo
Mkoani Shinyanga.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjla,
amesema serikali imeondoa kodi zote kwa wachimbaji wadogo zilizokuwa zikilalamikiwa
na wachimbaji pamoja na kampuni za uchenjuaji wa dhahabu lakini bado wizi
unafanyika tena kwa kiwango kikubwa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amikiri kwamba hana
elimu ya madini hivyo imekuwa vigumu kwake kudhibiti wizi huo lakini anaamini wizi na udanganyifu upo tena
kwa kiwango kikubwa.
“kiukweli sina elimu ya madini hasa kwenye upande wa uchenjuaji wa
dhahabu, naamini kuna wizi mkubwa wa madini haya ya dhahabu na taarifa zisizo
na ukweli”amesema Chalamila.
![]() |
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Wizara ya Madini na Viongozi wengine wa Wilaya ya Chunya wakisikiliza maelezo ya namna wizi unavyofanyika katika mitambo ya kuchenjua dhahabu. |
![]() |
Wachimbaji
wadogo wadogo wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauli ya wilaya ya
Chunya wakimsiliza Waziri wa Madini Doto Biteko
|
![]() |
Waziri wa Madini
Doto Biteko akitoa akieleza jambo wakati akitoa maelekezo ya namna ya kuifungia
kampuni ya uchenjuaji dhahabu ya Ntorah Gold and Diamond Ltd wilayani Chunya
|
No comments:
Post a Comment