Na Asteria
Muhozya, Dodoma
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki amemkabidhi rasmi
Majukumu ya Uwaziri wa Wizara ya Madini, Waziri Doto Biteko katika kikao
kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Waziri Kairuki
amemshukuru Waziri Biteko kwa ushirikiano aliompatia kwa kipindi chote alichokuwa
Waziri wa wizara hiyo na kueleza kwamba, kabla ya makabidhiano hayo, wamepata
wasaa wa kupitia kwa pamoja majukumu na vipaumbele vya wizara ikiwemo maeneo
muhimu yanayotakiwa kupewa msukumo.
Naye, Waziri
Biteko, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, amemshukuru Waziri
Kairuki na kumwelezea kuwa ni Waziri aliyekuwa mwalimu mzuri kwake kwa kipindi
chote alichokuwa Naibu Waziri.
Ameongeza,
Waziri Kairuki hakuwahi kumnyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kumtuma kutekeleza
majukumu mbalimbali nafasi ambayo ilimkomaza.
“ Waziri
hakuwahi kuninyima fursa, alinituma popote na nitaendelea kuhitaji ushauri wake
katika kutekeleza majukumu yangu,” amesisitiza Biteko.
Makabidhiano
hayo yamefanyika Machi 12, ofisini kwa Waziri Biteko Jijini Dodoma.
Waziri Biteko
aliteuliwa Januari 8, 2019 kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza
la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Waziri Biteko alichukua
nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki ambaye aliteuliwa kuwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.
Waziri wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah
Kairuki, akimkabidhi Nyaraka za majukumu ya Wizara ya Madini, Waziri Doto
Biteko.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Waziri wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah
Kairuki, akimkabidhi Nyaraka za majukumu ya Wizara ya Madini, Waziri Doto
Biteko.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Waziri wa Madini Doto Biteko na Waziri Waziri wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah
Kairuki, wakifurahia jambo mara baada ya makabidhiano. Katikati anayeshuhudia
ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
No comments:
Post a Comment