Na Issa Mtuwa, Songea
Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema
kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi
nzuri wanayoifanya.
Akiongea na waandishi
wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua
ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri
amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea
kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.
“Tunawapongeza sana
Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea
kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.
Naibu Wziri wa Madini
Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika
kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia
ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea
kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo
uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa
ujenzi unaendelea kwa kasi.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa
wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na
tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote
uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.
Nae Katibu Tawala wa
mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo
amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa
na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama
kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara
baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto
ulikuwa ni tatiizo.
Kituo cha Umahiri
Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika
maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo
la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala
mbalimbali madini.
No comments:
Post a Comment