Na Issa Mtuwa Dodoma
Nchi Wanachama wa
Maziwa Makuu zimetakiwa kushikamana kuunganisha nguvu katika kulinda na kusimamia
matumizi ya raslimali ardhi ikiwemo madini ili kunufaisha nchi hizo.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua mkutano wa Kimataifa wa nchi Wanachama wa Maziwa Makuu (International Conference on the Great Lakes
Region - ICGLR) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Machi 2019
katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.
Biteko amezitaka nchi
hizo kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti raslimali ardhi ikiwemo
madini na kujiwekea utaratibu utakao dhibiti shughuli za uzalishaji na biashara
ya madini ili raslimali hizo zinufaishe mataifa yao na zisitumike vibaya.
“Unganisheni nguvu
kwa pamoja, wekeni utaratibu utakao wafanya nchi wanachama kunufaika na
raslimali ardhi/madini. Jitahidini kuhakikisha raslimali hizo hazitumiki vibaya
kama ilivyo kubaliwa kwenye itifaki, hivyo lazima kuwe na utaratibu na sheria
kwa kila nchi namna ya kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini,” amesema
Biteko.
Naye, Mtaalam kutoka Wizara
ya Madini, Mhandisi Assah Mwakilembe amesema Mkutano huo unalenga kujadili na
kupitia mfumo wa udhibitisho wa mnyororo wa madini kwa lengo la kudhibiti
uzalishaji na biashara ya madini katika nchi za maziwa makuu kufuatia kuwepo tetesi
zilizo kuwa zinahusisha raslimali ardhi (Madini) na ufadhili wa vita katika
nchi za aaziwa makuu. (Region Certification Manual).
Akizungumza mara baada
ya kuwasilisha mada kuhusu marekebisho ya Sheria Madini ya Mwaka 2017 Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Madini, Edwin Igenge amesema kwa upande wa
Tanzania, imetekeleza itifaki ya pamoja ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu kama
ilivyo kubaliwa.
Ameongeza kuwa,
utekelezaji wa itifaki kwa Tanzania ni pamoja na marekebisho ya sheria ya Madini
ya Mwaka 2017 yaliyopelekea kuundwa kwa Tume ya Madini ambapo shuguli zote za
usimamizi wa raslimali madini zimepewa Tume ya Madini ambapo kabla ya hapo shuguli
hizo zilikuwa chini ya Kamishna wa Madini.
Igenge amesema
kuanzishwa kwa itifaki katika nchi za maziwa makuu kulitokana na tetesi za
uwepo wa matumizi mabaya ya raslimali ardhi ikiwemo madini ambapo kipato cha
raslimali hizo inasadikika kuwa zilikuwa zinatumika kufadhili shuguli za za
kivita katika nchi za maziwa makuu, hivyo kupelekea kuanzishwa kwa itifaki ya
pamoja kwa lengo la kudhibiti.
Mkutano huo wa
kimataaifa unahudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania, Burundi, Rwanda na
wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretariati ya nchi
wanachama wa Maziwa Makuu. Kwa upande wa Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Madini,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Shirikisho la
Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini Tanzania (TAMIDA), Tume ya Madini, Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO), Wakala wa Jiolojia na Utafiti
wa Madini (GST).
Katika mkutano huo, Waziri
Biteko aliambatana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini
Mhandisi Daivid Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria kutoka Wizara ya Madini Edwin
Igenge na baadhi ya maafisa kutoka wizara ya Madini.
![]() |
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akiongea na wajumbe wa mkutano wa kimataaifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu jijini Dodoma. |
Mjumbe kutoka Burundi Gerard Nayuburundi akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kimataifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu kwenye Hotel ya Morena Jijini Dodoma. |
No comments:
Post a Comment