Na
Asteria Muhozya,
Waziri wa
Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management
Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko
kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza
katika sekta ya madini.
Dkt. Gollmer
amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan
katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi
unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi
ambaye amekuwa akihamasisha watu wa
mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.
Pia, ameeleza
kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira
tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini
ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza
katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni
muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya
kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na
kampuni hizo.
Wengine
walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa,
Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri
Kungulu Kasongi.
![]() |
Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa
Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter
Gollmer.
![]() |
Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo
wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya
Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
![]() |
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources
Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni
Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
![]() |
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais
wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter
Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na
Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.
No comments:
Post a Comment