Na Issa Mtuwa, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Madini kwa utekelezaji wa Ujenzi wa Jengo
la Taaluma la chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Ujenzi wa Jengo la Ofisi za
Wizara ya Madini lilipo eneo la Mji wa Serikali Ihumwa, Jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa Machi 13, 2019 na Wajumbe wa Kamati hiyo
wakati wa kikao cha majumuhisho kilichofanyika kwenye jengo la wizara ya Madini
Ihumwa, mara baada ya kukagua majengo yote mawili na kupewa taarifa ya ujenzi
wake.
Wakiwa kwenye jengo
la taaluma la chuo cha madini, wajumbe wamepongeza na kuridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kupongeza SUMA
JKT kujenge jengo hilo.
Jengo la Taaluma ni
la ghorofa tatu lenye ofisi, vyumba vya kufundishia na ukumbi wa mikutano. Ujenzi
huo utagharimu jumla ya shilingi 2, 863, 161, 369.00 hadi kukamilika kwake na unatekelezwa chini ya chini ya Mradi wa
Usimamizi Endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP) kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Akizungumzia ujenzi
wa jengo la Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila
amewaeleza wajumbe wa kamati kuwa, ujenzi huo ulianza tarehe 4/12/2018 na
ulitakiwa kukamilika tarehe 31/01/2019, hata hivyo mkandarasi hakuweza
kukamilisha ndani ya muda huo kutokana na sababu mbalimbali. Prof. Msanjila
ameongeza kuwa, kwa kuzingatia ushauri wa msimamizi wa ujenzi huo, walifikia
makubaliano ya kumuongezea muda mkandarasi hadi kufikia tarehe 28/02/2019.
Prof. Msanjila
ameongeza kuwa, mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 80 na mwezi ujao wizara
itakuwa tayari kuhamia. Amesema ujenzi huo umegharimu Jumla ya shilingi Milioni
975,360,028.10 zitatumika katika ujenzi huo.
Naye, Waziri wa Madini Doto Biteko ameiambia
kamati kuwa, mkandarasi wa ujenzi huo, alipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha
ujenzi wake ili wafanyakazi wa Wizara hiyo waanze kulitumia. Waziri emeleza
kuwa wizara inaridhishwa na kasi ya mkandarasi katika ujenzi huo.
Biteko ameongeza kuwa,
wizara imedhamiria kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kuthibitisha
hilo wizara imemteuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimaliwatu, Nsajigwa
Kabigi ambae yupo muda wote wote eneo la ujenzi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Dunstan Kitandula amesema pamoja na wabunge kuipongeza wizara kwa
kazi nzuri, ameishauri wizara na mkandarasi wa ujenzi huo, Mzinga Holdings Company kujielekeza kwenye manunuzi ya vifaa
vinavyopatikana hapa nchini.
Wakichangia wajumbe
wa kamati hiyo, Joseph Musukuma na Ally Keissy wakichangia wakati wa
majumuhisho waliipongeza wizara na mkandarasi, hata hivyo, walishangaa muda
waliopewa na hatua iliyofikia, msukuma alisema ni kazi ya kupongeza na wameeleza pamoja na mkandarasi kutokamilisha
kazi yake kwa wakati bado utendaji wake wa kazi unaridhisha na kasi yake inaonekana.
Naye, Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo aliwaambia wajumbe wa kamati kuwa, ujenzi wa jengo hilo
la wizara unafanana ramani na wizara nyingine ikiwemo kiasi cha fedha
zilizotolewa na serikali zote zikiwa na kiwango cha shilingi Bilioni moja.
Amesema muda uliotolewa
ulilenga kutimiza azma ya wizara kuhamia eneo hilo kwa wakati. Aliwashukuru
wajumbe kwa ushauri wao na kueleza kwamba
kama wizara watauzingatia.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa na viongozi wa juu wa
wizara ya madini wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jingo la Wizara Ihumwa
Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na viongozi wa Wizara ya Madini wakiwa kwenye kikao cha majumuisho baada ya kutembelea miradi |
No comments:
Post a Comment