v AITAKA KUIWEZESHA GST KURAHISISHA MAISHA YA
WACHIMBAJI
Asteria
Muhozya na Samwel Mtuwa, Dodoma
Bodi ya Taasisi
ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imetakiwa kuiwezesha taasisi
hiyo kurahisisha maisha ya Wachimbaji Wadogo, wa Kati na Wakubwa kwa
kuhakikisha wanapata taarifa za tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa
na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizundua Bodi ya GST na kueleza kuwa,
shughuli za utafiti ni moja ya maeneo muhimu katika sekta ya madini kutokana na
kutoa uhakika kwa wachimbaji na hivyo kukidhi matarajio ya wadau.
Katika hatua
nyingine, Waziri Biteko ameitaka bodi hiyo kuhakikisha GST inapata Ithibati ya
maabara yake ikiwemo kutangaza huduma zinazotolewa na maabara hiyo ili
kuwawezesha wadau kuifahamu na kuitumia.
Aidha, ameitaka
bodi husika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sera, sheria na taratibu
zilizowekwa na kueleza kwamba, taasisi hiyo inao watendaji wazuri wa kuiwezesha
kutekeleza majukumu yake kiamilifu na kutumia fursa hiyo kumpongeza Kaimu
Mtendaji Mkuu wa GST Yokberth Myumbilwa, kwa kusimamia vema utendaji wa GST.
Naye, Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema taasisi hiyo ni kitovu cha sekta ya
madini nchini na kwamba ndiyo imeshikilia mstakabali wa wachimbaji wadogo, wa
kati na wakubwa.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Justinian Ikingura amesema bodi hiyo
inatambua umuhimu wa rasilimali madini katika kuchangia pato na kukuza uchumi
wa taifa ikiwemo kutambua nia na lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Amesema ili
kufikia lengo hilo, ni muhimu GST ikawezeshwa ipasavyo kupitia wizara ili
iongeze kasi na tija zaidi katika kutekeleza majukumu yake, hususan katika
maeneo ya kufanya utafiti na kukusanya taarifa muhimu za kijiosayansi za kubaini
maeneo yenye miamba yenye vishiria vyakuwepo madini ya kimkakati yanayohitajika
zaidi katika matumizi ya teknolojia ya viwanda vya kielekitroniki, zana za
utafiti wa mawasala ya anga na matumizi maalum katika viwanda vingine, ili
kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchini katika maeneo hayo.
“Kwa mfano madini lithium, cobalt na palladium
yanazidi kupata umuhimu wa pekee katika matumizi ya viwanda vya kimkakati. Hivi
majuzi takriba wiki moja iliyopita bei ya Palladium ilifikia kiasi cha dola za
kimarekani 1,600 kwa wakia na kuzidi hata dhahabu ambayo ikiwa karibu dola
1,300 kwa wakia moja. Lakini si wengi wanatambua madini ya Palladium ambayo
yako katika kundi la metali za Platinum, yaani Platinum Group Metals (PGM),”
amesisitiza Prof. Ikingura.
Ameongeza
kuwa, eneo jingine ni uboreshaji wa huduma za maabara za uchunguzi na upimaji
wa miamba na madini yake ili zikidhi viwango vya kimataifa, na hivyo kuvutia
wawekezaji katika sekta ya madini kutumia zaidi maabara za ndani ya nchini
badala ya kupeleka sampuli katika maabara za nje ya nchi, na hivyo kupoteza
fedha za kigeni.
Vilevile,
amesema ipo haja ya kuboresha na kuongeza thamani taarifa za jiofikizia na
jiokemia zilizo katika hifadhi au kanzidata ya GST ili ziweze kuwa na thamani
kubwa zaidi kwa taifa na kwa wawekezaji
katika sekta ya madini, suala ambalo
litaiweesha GST kuongeza maduhuli ya serikali kupitia wizara.
Mbali ya Mwenyekiti,
wajumbe wa bodi hiyo ni Abdulkarim Hamisi Mruma,
Emanuel Mpawe Tutuba, Bibi Bertha Ricky Sambo, Shukrani Manya, David R. Mulabwa
na Bibi Monica Otaru.
Bodi hiyo
imezinduliwa Machi 27, 2019 Makao Makuu ya GST, jijini Dodoma.
![]() |
Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto) akizungumza
na jambo wakati wa uzinduzi wa bodi ya GST . Kulia anayefuatilia hayo ni Mwenyekiti
wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingula.
|
No comments:
Post a Comment