Na Nuru Mwasampeta,
Licha ya kwamba Wizara ya Madini kuwa
miongoni mwa wizara nyeti katika kufikia uchumi wa viwanda, inakutana na
changamoto nyingi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa
Madini na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki katika mkutano wa hadhara na
wananchi wa jimbo hilo Tarehe 9 Machi, 2019.
Naibu Waziri Nyongo alizitaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na utoroshwaji wa Madini unaosababisha Taifa
kutokupata kodi stahiki, uwepo wa mikataba isiyolinufaisha Taifa, hali mbaya ya
wachimbaji wadogo na hali ya wachimbaji kufanya shughuli zao bila kuzingatia
suala zima la usalama.
Pamoja na changamoto hizo, Naibu
Waziri Nyongo alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilifanyia marekebisho
ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 mnamo mwaka 2017.
"Mimi pamoja na uongozi wote wa
wizara ya Madini tumepewa dhamana kusimamia sheria hiyo ili Madini yaliyopo
nchini yanufaishe Taifa na watu wake", alisema Nyongo.
Awali kabla ya mkutano huo, Naibu Waziri
Nyongo alifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili
katika eneo ambako ujenzi wa barabara unaendeshwa ili kukagua utekelezaji wa
ilani ya Chama Tawala cha CCM
|
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akiwasili katika eneo panakojengwa shule na kupokelewa
na Diwani wa kata ya Nyalikungu JosephBundara.
|
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akifuatilia hotuba ya Katibu wa CCM wa Wilaya ya Maswa
alipokuwa katika mkutano wa hadhara ili kusikilia na kutatua changamoto ya
wananchi wa wilaya hiyo
|
No comments:
Post a Comment