v Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia
watanzania kutokea Ihumwa
v Mkandarasi aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku
Tano
Viongozi
Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko
leo Machi 23, wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali
eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Akizungumza
baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia
watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia
kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa
kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara.
Vilevile,
Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya
mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na
wajeta wake.
Pia, amemshukuru
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana na
msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa
wakati.
Aidha, amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga
Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora
nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara imepanga
kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti ya aina
mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri ya
kuvutia.
Naye, Katibu
Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya Mzinga
Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi cha siku
Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika hatua
nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila.
Akizungumzia
mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa
wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na
kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia
katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa
kifedha.
Pia, ameeleza
kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini ya mable ambayo yamepatikana kutoka kwa
wachimbaji wadogo wa madini nchini.
Kwa upande
wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo Hamisi
Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani ya siku tano zijazo, jengo hilo
litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.
![]() |
Muonekano
wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la
Ihumwa.
|
![]() |
Waziri wa
Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa
tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua
maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara
|
![]() |
Waziri wa
Madini Doto Biteko katikati na Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakiangalia kitu wakati wa ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara, Ihumwa.
|
No comments:
Post a Comment