Na Issa Mtuwa, Tarime
Serikali imesema
itaufunga mgodi wa North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa
kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia
maji (topesumu) (Tailings Storage
Facility -TSF) ya mgodi huo kuelekea
kwenye makazi ya watu.
Hayo yamesemwa leo
machi 5, 2019 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo
kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa topesumu
(TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na baadae na wananchi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime kuzungumzia
hatima ya malipo ya fidia za wananchi waliohamishwa kupisha shuguli za mgodi.
Biteko amesema
serikali hairidhishwi na namna mgodi wa North Mara kwa jinsi wanavyo zingatia
swala la utunzaji wa maji yenye sumu kwenye (TSF) zao. Amesema serikali
inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja, na kwamba maisha ya mtu mmoja
ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.
“Naomba niseme ukweli,
tena kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye
sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya Dkt. John
Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu chochote. Thamani
yamaisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko kinachochibwa hapa. Nitoe rai kwa
mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu, hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo,
nitafunga mgodi mpaka pale mtakapo tekeleza jambo hili” alisema Biteko.
Kwa upande wa uongozi
wa mgodi umesema, utatekeleza agizo hilo na kwamba juhudi za kudhibiti topesumu
kuelekea kwenye makazi ya watu limepewa kipaumbele na kwamba ndani ya muda huo
litakuwa limekamilika.
Katika ziara hiyo,
Waziri Biteko aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna
wa Madini Mha. David Mlabwa na Afisa Madini mkoa wa Mara Mha. Nyaisara Mgaya,
wengine ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara wakiongwa na mwenyekiti
wake ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Mara bwana Adam Kigoma Malima.
Ziara hiyo inafuatia
vikao mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala
mbalimbali yanoyo husu mgodi huo likiwemo swala la udhibiti wa maji yenye sumu
(topesumu) yanayo lalamikiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi huo, kikao
cha kwanza kilifanyika Januari 19, chini ya makatibu wakuu wa wizara saba ((Madini,
Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi, TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji)) ambapo
serikali ilitoa miezi nane kutekeleza maagizo yaliyopewa.
![]() |
Waziri wa Madini Mhe.
Doto Biteko wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekiiti wa kamati ya ulinzi na
usalama na mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kwanza kushoto akitoa taarifa
fupi ya hali ya mkoa wake wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tarime.
![]() |
Waziri wa Madini Mhe.
Doto Biteko akionyesha kwa kuuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa TSF
mpya, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya
Tarime.
No comments:
Post a Comment