Na Issa Mtuwa, Tarime
Waziri wa madini Mhe.
Doto Biteko ameonyesha kukerwa na tabia zinazofanywa na uongozi wa juu wa mgodi
wa Acacia North Mara kwa serikali kwa
kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyo andaliwa baina ya pande hizo
mbili, licha ya baadhi ya vikao kuongozwa na Waziri wa Madini lakini viongozi
wa juu wa mgodi ambao ndio wafanya maamuzi na watekelezaji wa maagizo ya
serikali wamekuwa wakishindwa kuhudhuria.
Biteko amesema hayo
wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara jana Machi 5, 2019 katika
kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime
ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya
kikazi kwenye migodi ya North Mara na Buhemba. Biteko amesema anakerwa na tabia
za uongozi wa mgodi huo kwa kushindwa kuhudhuria mara kwa mara mikutano
mbalimbali ya ndani na ile ya hadhara badala yake wamekuwa wakituma wawakilishi.
“Kuanzia leo, haki ya
mungu, haki ya mungu, haki ya mungu, mimi Waziri wa Madini leo ni siku ya
mwisho kukaa na hawa wawakilishi kwenye vikao, hasa kama hivi vinavyo husu
hatima ya maisha ya watu alafu wafanya maamuzi hawahudhurii. Niwambie ukweli nasikitishwa
sana na tabia hii. Hawa walipo sio saizi yangu, kama ni hawa hata mimi ningewaleta
maafisa wa wizara tena wale wanaolingana na hawa.
Wanataka
wawepo hadi afike Rais…!? nendeni mkawambie kwenye ngazi ya Wizara mimi ndio
wamwisho katika kufanya maamuzi, kama mimi nipo kwa nini wao wasiwepoo…!?
nyinyi mliokuja hapa nendeni mkawaambie hii ni mara ya mwisho wasifikiri
serikali hii wanaweza kuiweka mfukoni, haikubaliki, hii tabia lazima ifike
mwisho” alisema Biteko huku akisikitika sana.
Amesema kwa ujumla
hafurahishwi na namna mambo yanavyokwenda mgodini hapo ukilinganisha na migodi
mingine. Mgodi wa North Mara umezungukwa na matatizo mengi sana yakiwemo ya
malipo yafidiaza wananchi, utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi
ya wananchi.
Waziri
wa Madini Mhe. Doto Biteko akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kijiji cha Nyamongo wilayani
Tarime.
|
No comments:
Post a Comment