Ø ASEMA
ATAKAYEKAMATWA NA TANZANITE MARUFUKU KUINGIA TENA NDANI YA UKUTA.
Ø ATAKA
MINADA YA TANZANITE ILIYOSIMAMISHWA SASA IANZE.
Ø SUMA JKT msitucheleweshe,
ifikapo
Aprili mwaka huu jengo liwe limekamilika. Jengo hili la Kituo cha Pamoja cha
Biashara ya Madini litajengwa na SUMA JKT kwa gharama ya shilingi 1,148,
259,500.
Ø Tunafunga CCTV camera kuzunguka ukuta. Lengo la uwekaji wa mitambo hii
ni kuimarisha ulinzi kwa ajili ya rasilimali na watu waliomo na
wanaoingia ndani ya ukuta. Tunataka tukiwa Dar es Salaam na Dodoma tuwaone. Rai
yangu kwenu ni kila mtu awe mlinzi wa rasilimali madini na kwa upande
wafanyabiashara wapende kununua katika mkondo sahihi madini yao ili kuepuka
usumbufu.
Ø Tarehe 30 Januari 2019 nilisaini Kanuni za Mirerani Controlled Area.
Nakuagiza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Kamati ianze kazi tuanze kusimamia Kanuni
hizi.
Ø Tumekuja kumkabidhi mkandarasi site hakuna kulala mpaka madini
yalinufaishe taifa.
Ø Mkandarasi wa CCTV nakukabidhi kazi hii nataka ufanye kazi yenye ubora
na kumaliza ndani ya Mkataba tuliokubaliana bila kuongeza hata sekunde.
Ø Tulieni tunakuja na utaratibu wa mashine. Wizi ni lazima tuutoe
kwenye fikra zenu.
Ø Wakati ukuta huu unajengwa kulikuwa na siasa nyingi. Wapo
waliouita jela lakini leo mapato yameongezeka mnalipa kodi vizuri. Tunakwenda
kuondoa vikwazo kwenye biashara ya madini. Mtalipa mrabaha usiozidi asilimia 7.
Deni limebaki kwenu.
Ø Suala kujengwa ukuta lilikuwepo tangu mwaka 2002 lakini haukujengwa.
Ametokea mzalendo Rais Magufuli tumejenga. Asingekuwa yeye ingebaki hadithi
nyingine.
Ø Nitawashangaa sana baada ya jitihada hizi tunazozifanya mapato
yakishuka. Mkuu wa Mkoa wasimamieni hawa huku mkiwalea.
Ø Jengo la biashara ya madini limejengwa mahususi ili kurahisisha
uthaminishaji wa madini pindi yanapovunwa hapa ndani.Ma broker tumewajengea
nyumba hii hapa tuheshimu taratibu.
Ø Jengo hili la biashara na uthaminishaji litatumika kuwakutanisha
wafanyabiashara wadogo na wenye madini ili kuweza kufanya biashara sehemu
salama na kwa uwazi. Kama alivyosema Katibu Mkuu, jengo hili limegharimu
shilingi milioni 85.
Ø Tanzania Tumegeuka kuwa darasa kwa jirani zetu na nchi nyingine
kutokana na namna tunavyosimamia Sekta ya madini. Watu wa mataifa wanakuja
kujifunza lakini pia Tunapata mialiko mingi kutoka nchi mbalimbali ili
tuwaeleze namna tunavyosimamia rasilimali hii.
Ø Tutumie madini yetu kubadilisha maisha yetu. Tunataka siku moja watoto
wa Simanjiro wasome kwenye shule nzuri, watumie barabara nzuri, akina mama
wapate huduma za afya sehemu nzuri. Haya ndiyo mambo tunayoyataka. Siasa
nyingine siyo agenda ya watanzania.
Ø Tanzania ni nchi ya 3 Afrika kwa kuzalisha dhahabu, ya pili Afrka kwa
madini ya vito na ya 18 duniani kwa kuzalisha dhahabu lakini utajiri huu wa
madini na maisha ya watanzania havifanani.
Ø Minada ya Tanzanite iliyosimamishwa sasa ianze.
Ø Chama Cha MAREMA unganeni,tukigundua hamna msaada tutawaacha.
Ø Hatutaki kukwamishana,tunataka kusimamia sekta..Wachimbaji acheni
majungu, toeni taarifa za kweli.
Ø Hatutawatoza fedha nyingi lakini mtatuonesha vitambulisho. Natoa
maelekezo kuanzia leo tozo za kiingilio zitatozwa kwa wale wanaofanya kazi.
Ndani ya mgodi watalipa shilingi elfu 50,000 kwa mwaka, Mabroker watalipa
shilingi elfu 30,000 kwa mwaka na wana Appolo, wafanyabiashara wadogo kama wachekechaji,
mama lishe watalipa shilingi 20,000 kwa mwaka.
Ø Naomba Wizara ya Kazi kupitia Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (
WCF) na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuja kujifunza na kutengeneza muundo
ambao unaendana na aina ya kundi hili ili kuweza kulihudumia kundi hili la
wachimbaji wadogo wa madini.
Ø Katika mkutano wa wadau wa tarehe 22 Januari, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli pamoja na mambo mengine
alisisitiza kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara ya Madini Tanzania na pia
kuimairisha usalama. Tuliagizwa kiualisia kuanza mara moja kuweka mifumo ya
kidigitali kuzunguka ukuta.
ALIYOYASEMA
MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI
Ø Mkoa wa Manyara ni mkoa mkubwa wenye Tanzanite ambayo haipo popote
duniani. Unapokuwa Mkuu wa Mkoa kama huu lazima uweze kudhibiti Tanzanite.
Nataka nikamwambie Mhe. Waziri tuna madini mengi zaidi ya Tanzanite.
Ø Kwenye madini lazima nibanane na wewe. Nisipodhibiti sina cha kumwambia
Mhe. Rais. Tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha kodi zinapatikana.
Babati tuna rubi ya kutosha. Nataka nikwambie ifanye Babati kuwa Makao Makuu ya
Madini nchi nzima.
Ø Mhe. Waziri kazi yetu ni kusimamia mnayoyapitisha juu ili yasipotoshwe
na yatekelezwe kwa Mujibu wa Sheria.
Ø Mhe. Rais alituelekeza tupitie na kukubaliana kuweka mazingira mazuri ya
kuboresha Tanzania kupitia sekta hii. Tulikaa kujadili mabadiliko makubwa. Nina
hakika mabadiliko makubwa yanakuja.
Ø Mhe. Waziri tumeshakubaliana na wadau hawa mambo mengi. Tunataka kuona
mengi kutoka kwao.
Ø Ni matarajio yangu kuwa shughuli nyingi zitafanyika ndani ya jengo la
Kituo cha Biashara.
Ø Nakipongeza Chama Cha Marema kwa kufanya kazi nzuri. Ukipingana na
Serikali hakuna unachoweza kufanya. Hakuna aliye juu ya serikali.
ALIYOYASEMA
MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI,
DUSTAN KITANDULA
Ø Mhe. Rais ameonesha uungwana, mpira uko kwenu. Hisani pekee kwake ni
ninyi kulipa kwa kuonesha kwa vitendo. Yale yaliyokuwa yakiwakwaza yameondoka,
mlipe kodi.
Ø Tumewaona mkiwa katika maandamano ya kumuunga mkono Rais. Kikao cha
Januari 22 kilionesha dhamira ya Rais na aliahidi kutekeleza kero zenu
ndani ya kipindi kifupi. Tuliletewa miswada kufanya mabadiliko.
Ø Nampongeza Rais kwa kuondoa vikwazo kwa wachimbaji wadogo. Serikali
imedhamiria kuhakikisha sekta hii inalinufaisha taifa.
ALIYOYASEMA
MBUNGE WA SIMANJIRO JAMES OLLE MILLYA
Ø Kuwepo kwa ukuta huu hakumaanishi hakuna majirani. Kwa mujibu wa Sheria
na taratibu zake nakuomba Mhe Waziri migodi hii isaidie
jamii. Wanaofanya uchimbaji wakumbuke vijiji vya jirani.
Ø Baada ya kujengwa ukuta bado wanapanga mistari mirefu. Wanaongia
ndani wakaguliwe mapema.
Ø Bado kuna changamoto kwako Mhe. Waziri na Katibu Mkuu ikiwezekana
muwaletee maji.
ALIYOYASEMA
MWENYEKITI WA MAREMA, JUSTIN NYARI
Ø Mhe. Rais ameweka alama ambayo haitapotea, alama ambayo itakumbukwa kwa
vizazi na vizazi.
Ø Ujenzi wa kituo cha pamoja cha biashara ni mwanzo mzuri kwetu na
mkoa wetu na nchi yetu, wachimbaji wako tayari kushirikiana na serikali.
No comments:
Post a Comment