Ø NI
KUFUATIA KUPUNGUZA KODI ZA MADINI NA KUSIKILIZA KERO ZAO
Ø WAAHIDI
KULIPA KODI
Maandamamo
hayo yaliyofanyika Februari 16, yalihusisha wadau wote wa madini ya Tanzanite
wanaofanya shughuli za uchimbaji ndani ya ukuta wakiwemo wachimbaji wadogo, wa
Kati na Wakubwa, yakilenga kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kupunguza
kodi za madini, kusisitiza suala la uanzishwaji wa masoko ya madini na
mwongozo wa uongezaji thamani madini
v ALIYOYASEMA
MKUU WA MKOA WA MANYARA, ALEXANDER MNYETI
Mhe. Rais ametuagiza mlipe kodi kwa hiari.
Msipofanya hivyo mtalipa kwa nguvu. Lipeni kodi.
Ø Nimepokea maandamano yenu na tutaandaa barua Maalum kwenda kwa Mhe. Rais
kufikisha salam zenu.
Ø Mnajua safari ya tulikotoka, tulipofika na tunaweza kutengeneza njia
nzuri ya tunakotaka kufika. MAREMA inakwenda vizuri.
Ø Mirerani acheni umbeya, kuna uongo mwingi, punguzeni uongo taarifa zenu
zinatupotosha.
Ø Mnajichonganisha wenyewe na serikali. Waajiri mnawatelekeza wafanyakazi
wenu wakiugua wanakuwa mzigo wa serikali.
ALIYOYASEMA
MWENYEKITI WA MAREMA, MKOA WA MANYARA, JUSTIN NYARI
Ø Maandamano haya yanalenga kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuondo
kodi ambazo hazikuwa rafiki kwa wachimbaji.Tunampongeza Mhe. Rais kwa kupeleka
bungeni Muswada kwa hati ya dharura, ujenzi wa masoko ya madini na
mwongozo wa uongezaji thamani madini.
Ø Wachimbaji wako tayari kushirikiana na serikali kukuza uchumi
kupitia sekta ya madini.
ALIYOYASEMA
MBUNGE WA SIMANJIRO, JAMES OLLE MILLYA
Tunampongeza Rais kwa kuondoa VAT ya
asilimia 18 kwenye sekta. Ameacha asilimia 7 tu huu ni upendo wa pekee.
Baada ya Januari 22 Mkuu wa Mkoa
aliitisha kikao Januari 25 na migodi yote imeanza kufanya kazi na matunda
yameanza kuonekana.
ALIYOYASEMA
MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO, MHANDISI ZEPHANIA CHAULA
Ø Kama Mhe. Rais amewaheshimu na ninyi mumheshimu, heshima hiyo ni kulipa
kodi.
ALIYOYASEMA
MWAKILISHI WA TANZANITE AFRIKA KWA NIABA YA WACHIMBAJI WA KATI, WILFRED MUSHI
Ø Tunampongeza Mhe.Rais, kwa mara ya kwanza ameondoa kero za wachimbaji wa
Kati ambazo hazipishani sana na wachimbaji wadogo.
Ø Nuru ya Tanzanite imenga'rishwa,
Mirerani sasa inakwenda kutengeneza
tanzanite mpya.
ALIYOYASEMA
MWAKILISHI WA TANZANITE ONE, FEISAL SHABHAI
Ø Tunampongeza Rais Magufuli kwa kutambua uwepo wetu, kusikiliza kilio
chetu na kuondoa changamoto zetu.
Ø Tunatambua maendeleo yanayotarajiwa kutokana na rasilimali hii ambayo
lengo ni kuwanufaisha watanzania na vizazi vijavyo viweze kuishi katika
mazingira salama.
ALIYOYASEMA
MWAKILISHI WA TAMIDA, HUSSEIN GONGA
Ø Tulikuwa na tashwishi kubwa juu ya kufanya biashara ya madini. Mhe Rais
alisikia kilio cha wachimbaji na dealers.
Ø Hawezi kuwepo mnunuzi bila mchimbaji, tulikuwa na changamoto ya
kusafirisha madini ghafi.
Ø Rais Magufuli ameondoa kodi ya VAT ya asilimia 18, ilikuwa kero kubwa.
Ø Mhe. Rais hajapoteza, mafanikio atayaona tunamhakikishia. Biashara
ya madini sasa inakuwa nzuri.
ALIYOYASEMA
MWAKILISHI WA BROKER,
Ø Tunampongeza Rais kwa suala la ujenzi wa masoko ya madini nchi nzima,
serikali itakusanya kodi ya kutosha.
Ø Niwaombe Ma broker, kufanya uthamini wa madini, sitamwombea radhi broker
yoyote atakayevunja sheria.
ALIYOYASEMA
MWAKILISHI WA WANA APOLLO
Ø Tunampongeza Rais Magufuli kwa kututambua wana Appolo na kutupa nafasi ya
kuwasilisha kero zetu. Tunaahidi kushirikiana katika nyaja zote. Wana Appolo
ndiyo wachimbaji wa tanzanite.
Ø Tunayo sababu ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, leo wana Appolo
tunapewa vipaza sauti. Kwa muda mrefu wana Appolo hawakuwa na sehemu ya kuzungumza.
No comments:
Post a Comment