Na
Nuru Mwasampeta,
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo amewataka watumishi wa wizara kuhakikisha wanatoa
huduma stahiki kwa watanzania ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano
ya Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Aidha, amewataka
watumishi hao, kila mmoja kulingana na majukumu yake kujipima utendaji wake binafsi kabla ya
kungoja vipimo vilivyopo kwa kuzingatia miongozo na taratibu za Utumishi wa
Umma.
Naibu Waziri Nyongo,
ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua Mkutano wa Wafanyakazi wa Wizara kwa
niaba ya Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyekuwa katika utekelezaji wa majukumu
mengine ya kitaifa.
Aidha, Nyongo
amewaeleza watumishi hao kuwa wanao wajibu wa kuzingatia dhana nzima ya kuongeza
ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya
Taifa na watanzania kwa ujumla.
Pamoja na rai ya kila
mtumishi kujipima utendaji wake, Nyongo amewakumbusha kuzingatia matumizi ya
Opras katika kutekeleza na kujipima namna kila mmoja anavyotekeleza majukumu
yake.
Amesema Opras ni hitaji la kisheria kila mmoja hanabudi kulizingatia.
“Wote tnafahamu kuwa
ipo miongozo mbalimbali inayotumika katika utendaji wetu wa kila siku hivyo ni
rai yangu kuwa tuizingatie ili kutoa huduma stahiki kwa watanzania kwa ufanisi
na viwango vinavyotakiwa.” Alisisitiza.
Aidha, Nyongo
alieleza wajibu wa Wizara kwa kuzingatia miongozo iliyopo ikiwa ni pamoja na kuweka
mazingira mazuri ya kazi yatakayowawezesha watumishi wake kutekeleza majukumu
yao ipasavyo.
Pamoja na hilo,
alikazia suala la kuwaendeleza watumishi, kuwajengea uwezo katika kazi zao
pamoja na kushughulikia na kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao
ya kazi.
Zaidi ya hapo, Nyongo
alisisitiza suala la kuimarisha mawasiliano baina ya watumishi wa wizara lakini
pia mawasiliano baina ya wizara na taasisi zilizo chini ya wizara na wadau wote
wa sekta ya madini ili kuongeza ufanisi hatimaye kuongeza tija katika utendaji
wa wizara.
Kuhusu kuzingatia
suala la afya za watumishi, Nyongo ameipongeza wizara kwa kuratibu mara kwa
mara suala la upimaji wa afya kwa hiari kwa watumishi wake na kutoa rai kwa
kila mmoja kutumia fursa hiyo na kujitokeza kupima afya zao kwa hiari.
Kutokana na uwepo wa
wastaafu katika mkutano huo, Nyongo alitumia fursa hiyo kuwapongeza sana
wastaafu watano walijumuika katika mkutano na hafla fupi ya kuwaaga na
kuwatakia maisha mema katika hatua nyingine ya maisha.
Kwa uande wake,
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Nsajigwa Kabigi kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila alisema mkutano
huo umelenga katika kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ya wizara ili
kupata mwelekeo wa namna bora ya kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu na
shughuli za kila siku za wizara pamoja na kubadilishana mawazo, kufurahi pamoja
na kuwaaga wastaafu.
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali
yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha
Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali
yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha
Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali
yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha
Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu
No comments:
Post a Comment