Na
Asteria Muhozya,
Waziri wa
Madini Doto Biteko amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Jervois Mining
Limited ya Australia ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Nikel-
Colbat, Kabanga.
Akizungumza
katika kikao hicho, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu kufuatwa kwa Sheria
na taratibu kwa wenye nia ya kuwekeza katika Sekta ya Madini na kueleza kuwa,
kwa upande wa Wizara, inafanya jitihada za kuondoa urasimu kwenye uwekezaji
katika sekta husika.
“Tunataka mwekezaji
mwenye nia anapoonesha dhamira ya kuwekeza baada ya taratibu zote kukamilika
basi aanze mara moja,” amesema Waziri Biteko.
Akizungumza
katika kikao hicho mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo Balozi Mstaafu Andrew
Mcalister, amesema kuwa, nchi ya Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa
madini ya Colbat kutokana na ubora wake na mazingira ya uwekezaji yaliyopo
nchini ikiwemo uwazi.
Mbali na
Waziri Biteko, wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo, na wataalam wengine wa wizara.
Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia Brye Croker.
|
Baadhi ya Wataalam wa Wizara ya Madini
wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Madini na wawakilishi wa kampuni ya Jervois
Mining Limited.
|
No comments:
Post a Comment