Na Samwel
Mtuwa, Mwanza
Mchakato wa kuondoa Mlolongo wa Kodi na Tozo kwa wachimbaji Wadogo wa
Madini upo katika hatua za mwisho na ndani ya muda mfupi ujao, baadhi ya kodi
na tozo hizo zitafutwa katika Sekta ya Madini.
Hayo yamesemwa Februari 11, 2019 na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati
akifungua Warsha kuhusu namna ya kuanzisha masoko ya madini nchini inayofanyika
Jijini Mwanza.
Warsha hiyo inayolenga katika kutoa elimu ya namna ya kuanzisha masoko ya
madini imeanza leo na itafanyika kwa siku mbili hadi Februari 12, 2019
ikiwashirikisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa na Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo.
Waziri Doto ameeleza, warsha hiyo ni muhimu kwa wizara nan
nchi kwa ujuml kutokana na lengo ililojiwekea
wizara hivi sasa ya kuhakikisha mchango wa sekta ya madini kwenye Uchumi na
maisha ya wananchi unaongezeka.
Ameongeza kuwa, ana imani kwamba kwa kuondoa baadhi ya tozo na kodi kwa
wachimbaji wadogo zitawezesha kuziba mianya ya utoroshaji wa madini na hivyo
kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa.
Waziri Biteko amefafanua kuwa, Mchakato wa kuandaa Kanuni za Masoko ya
madini umezingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka nchi zenye
masoko ya madini.
Ameeleza kuwa, Halmashauri zinaowajibu wa kuendelea kuwajenga, kuwalea,
na kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa sababu mazao yao ndio yanayotegemewa
kuuzwa katika masoko hayo.
Ametaka njia pekee ya kujibu na kutolea ufanunuzi wa taarifa potofu ni
kutumia maelekezo yaliyopo katika sheria ya Madini ya 2010 na Marekebisho yake
ya 2017.
“Pamoja na changamoto zilizopo kwenye usimamizi wa sekta ya Madini
nchini namshukuru Mungu kwani rasilimali hizi hazijageuka kuwa balaa,” amesema
Biteko.
Katika hatua nyingne, amesema kuwa, Maafisa madini watakaokuwa kikwazo katika
uanzishwaji wa masoko ya madini watachukuliwa hatua za kisheria.
Wadau katika warsha hiyo ni kutoka Mikoa ya Mwanza Dodoma, Arusha,
Geita, Shinyanga, Mara, Manyara, Kagera, Tabora, Singida, Mbeya, Morogoro,na
Ruvuma.
Warsha hiyo imeandaliwa na wizara ya Madini kwa ushirikiano na Taasisi
ya Uongozi.
Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya
pamoja na wadau wanaoshiriki Warsha ya kuanzisha masoko ya Madini Nchini.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na
baadhi ya Watendaji Waandamizi wa Wizara na Wadau wa warsha hiyo, mara baada ya
kuifungua.
Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya
pamoja na wadau wanaoshiriki Warsha ya kuanzisha masoko ya Madini Nchini.
No comments:
Post a Comment