Na
Rhoda James,
Waziri wa Madini,
Doto Biteko amemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick Exploration
Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL) uliodumu kwa muda mrefu.
MTL ambaye ni
mlalamikiji alikuwa anadai kulipwa kiasi cha Dola za Marekani 10,000 na Kampuni
ya BEAL.
Akisuluhisha mgogoro
huo Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya BEAL kumlipa mlalamikaji kwa kuwa vibali
vyote vinaonesha kuwa anastahili kulipwa.
Kikao hicho
kimefanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 jijini Dodoma katika Ofisi ya Waziri wa
Madini, Doto Biteko.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhD3eXRYjmp3xA6vTriTwMmYdJL83syLtbZdR1A9l1iooLF1Wgp-jm_00eXpMY6zPgV964uP9hkdAu9R8nqVPczAwzERcZcIseqGNyqnp3FlI5jtaH_Y_Mjj_1SQD8hl3aHExQvIL3bhS4/s640/Pic+1.jpg) |
Waziri wa Madini,
Doto Biteko akishuhudia Mwakilishe wa Kampuni ya Barrick Exploration African
Limited (BEAL), Janet Lekashingo akipeana mkono na mmiliki wa kampuni ya
Megagems Tanzania Limited (MTL) baada ya kufikia mwafaka wa mgogoro wao wa MTL
kulipwa haki yake.
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSfFNNwUf3NtcPw3l2qUnQpiHtVmReF1LnnuBGkUPSiUBbrgZMKsgYUDENOLcNZWxfDTR5p2Y5v_w1ESbhMGKCdRBVNg81DaiCzFoZm1oP1_9EsU9z1DSy3X-Zn1f8AR3oIB08OCvlJP4/s640/Pic+2.jpg) |
Kamishna wa Madini,
Mhandisi David Mulabwa (wa kwanza kushoto) akifatilia kikao cha kusuluhisha mgogoro kati ya Kampuni
ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL).
Wengine katika picha ni Mwanasheria wa Wizara, Godfrey Nyamsenda (wa pili kushoto),
Mwanasheria wa Novelty Advocate Joseph Asenga na Mmiliki wa Kampuni ya MTL,
Suleiman Nasib.
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSnS9EFOGHRkQMxJoTXL-h_EIjSP1vi_4XVxFMZADQQN6NooSEEgcyn8MyF4K2umeFyyIZXkP5EGG2XDHcGnngxH2fsfANMqHYob2bzBypjY_EwfwcTrqJr-dQ8wgQgFI70I8qmBheg-Y/s640/Pic+3.jpg) |
Mwakilishi wa Kampuni
ya Barrick Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo akimkabidhi
Waziri wa Madini, Doto Biteko nyaraka kwa ajili ya kupitia kabla ya kumaliza
Mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL)
na Megagems Tanzania Limited (MTL).
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvbzaUPAhVAHdxMKY6CT2vtr8puL5QdgR6S9-_oqY9XO1CaJ4E27O1d8dkKNEZ6X1xkW6WESu4tN2oyuJu_LQC9euUHuxoKMPMTZ5t73aTEwtUeXeCNAHV3uIdzyNWDsz_cVpsZ7uPNzo/s640/Pic+4.jpg) |
Waziri wa Madini,
Doto Biteko akipitia nyaraka iliyokabidhiwa kwake na Mwakilishe wa Kampuni ya
Barrick Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo (hayupo pichani)
kabla ya kumaliza mgogoro kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited
(BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL).
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUTOcHlkQohIBgaj0slNQknsc8prmS-fDcWB9_-nfBYYB37gciNJX-Bq6Lu3Bo-F6ZpCJQLsV-yrFexqXjTVchbxYXN3g0-z1ThGhj_ZvO_HzDt-oYB_WoBQ_Tyc59jxDqkz3hVo2_CQc/s640/Pic+5.jpg) |
Mliliki wa Kampuni ya
Megagems Tanzania Limited (MTL), Suleiman Nasib (wa kwanza kulia) akimsikiliza
Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) wakati alipokuwa akisikiliza
kesi iliyokuwepo kati yake na Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited
(BEAL). Wengine katika picha ni Wanasheria kutoka Novelty Advocate Joseph
Asenga na Godfrey Nyamsenda kutoka Wizara ya Madini.
|
No comments:
Post a Comment