Na Nuru Mwasampeta,
Waziri wa Madini,
Doto Biteko leo tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kampuni inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya
bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus katika Ofisi za Wizara
ya Madini zilizopo jijini Dodoma. Kikao chake
pia kilishirikisha Mkurugenzi wa Sera na
Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mhandisi Migodi Mkuu kutoka
Tume ya Madini, Conrad Mtui pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Madini. Lengo
la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Tanzaplus Minerals kwa kushirikiana na
kampuni nyingine ya AIMGROUP kutambulisha teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa
uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini. Waziri Biteko aliitaka kampuni ya
Tanzaplus kuendelea kufanya utafiti zaidi juu ya mfumo husika kwa kushirikisha
wadau mbalimbali kabla ya kuwasilisha
pendekezo lake Serikalini.
Waziri wa Madini, Doto
Biteko (kushoto) akizungumza na watendaji wa kampuni inayojishughulisha na
uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya
Tanzaplus. Waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka
Wizara ya Madini, Augustine Ollal, na Upendo Fatukubonye na Hamis Mhando ambao
ni watendaji kutoka kampuni ya Tanzaplus.
Mkurugenzi kutoka
kampuni ya Tanzaplus, Hamis Mhando (kulia) akielezea jinsi teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa
uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini inavyofanya kazi.
Waziri wa Madini, Doto
Biteko akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Wataalam kutoka
Wizara ya Madini wakinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Waziri
wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment