Na Nuru Mwasampeta,
Dodoma
Waziri wa Madini, Doto
Biteko ameitaka kampuni
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini
ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One kutokusita kuwasiliana naye pindi wanapokutana
na changamoto katika utekelezaji wa mradi wao.
Aliyasema hayo jana tarehe 15 Januari, 2019 katika kikao chake na
watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha, Biteko alisema
kuwa maombi yote ya leseni kubwa za uchimbaji wa madini zinawasilishwa katika
baraza la Mawaziri ili kuweza kuridhiwa baada ya wawekezaji kuonesha nia na kuwasilisha
maombi ya leseni hizo.
Biteko alikiri kuwa
anao uelewa wa kile kinachoendelea katika uwekezaji huo kutokana na
ushirikishwaji alioupata kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah
Kairuki kupitia vikao mbalimbali alivyoshiriki.
Akizungumzia lengo la
ujio wao katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium One,
Frederick Kibodya alisema ni kuelezea maendeleo waliyofikia katika uwekezaji
huo pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Madini.
Alisema, uteuzi huo
umelenga katika kukuza sekta ya madini ikiwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa
madini ya uranium, “Tunaimani kubwa kwako na tunamshukuru Mungu kwa kukupa
nafasi hii” alisema Kibodya.
Akizungumzia
uwekezaji uliofanyika mpaka sasa katika mradi huo alisema ni kiasi cha dola za
kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) kutoka mradi ulipoanza mwaka 2009.
Akizungumzia manufaa
ya mradi huo Kibodya alisema ni pamoja
na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Alisema madini hayo yakichimbwa
yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolijia mpya nchini.
Mradi utasaidia
katika kuongeza ajira nchini. Aliendelea kufafanua kuwa kwa kipindi cha ujenzi
wa mradi wanatarajia kuajiri watanzania 1600 kwa kipindi cha miezi kumi na
nane.
Aidha, alibainisha
kuwa kutakuwepo na uzalishaji wa ajila zisiso rasmi kiasi cha watu 4500 wakati
wa ujenzi na 2300 pindi uzalishaji utakapoanza.
Alisema, mradi
utasaidia katika kuhamisha utaalamu kutoka kwa wawekezaji kwenda kwa wazawa na
mradi umelenga katika kutoa elimu ya ajira na utaalamu kwa wazawa.
Pia Kibodya alisema,
mradi unatarajia kuliingizia taifa pato la kiasi cha dola za kimarekani milioni
220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho kitakuwa
kikibadilika kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Mradi wa uchimbaji
madini ya uranium katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali
ya Tanzania na Mbia wa kampuni ya Mantra anayejulikana kama Rosatom.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akisalimiana na Mkurugezni Mkuu wa kampuni ya Uranium
One Holdings N.V, Vladimir Hlavinka mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa
mazungumzo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick
Kibodya.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya Mantra, Fredrick Kibodya akichangia mada katika kikao baina ya wizara na
kampuni ya Uranium One Holdings N.V ofisini kwa waziri jijini Dodoma.
|
No comments:
Post a Comment