Na
Asteria Muhozya,
Waziri wa
Madini, Doto Biteko leo Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na Kampuni ya
madini ya Uranium ya Mantra Tanzania kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo baina
ya pande hizo mbili.
Kikao hicho,
kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na Mzee Mchata wakati wa mkutano wa Kisekta
ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wakati
akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao hicho, Rais
Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba amekuwa na mgogoro na
kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na bado hajapata suluhu.
Akijibu kero
iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Madini kuhakikisha
mgogoro huo unafikia mwisho.
Sehemu ya
Wataalam wa wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao cha
kusuluhisha mgogoro kati ya kampuni ya Mantra na Mzee Eric Mchata. Kutoka kulia
ni Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma, Kamishna wa Madini
Mhandisi David Mulabwa na Afisa Sheria wa Wizara ya Madini, Joseph Nyamsenda.
Waziri wa
Madini Doto Biteko akimweleza jambo Mzee Eric Mchata wakati wa kikao cha kusuluhisha
mgogoro baina yake na kampuni ya Mantra Tanzania.
Waziri wa
Madini Doto Biteko akimsikiliza Mzee Eric Mchata (kushoto) wakati wa kikao cha
kusuluhisho mgogoro baina yake na Kampuni ya Madini ya Uranium ya Mantra
Tanzania.
No comments:
Post a Comment