Na
Nuru Mwasampeta,
Waziri wa Madini,
Doto Biteko amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga, ofisini kwake
jijini Dodoma.
Biteko ameshukuru Dkt.
Mafwenga kwa kuonesha nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata cheti cha
mazingira baada ya kubainisha njia bora za kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata
uelewa juu ya uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza katika
kikao hicho kilichofanyika Januari 28, 2019, Dkt. Mafwenga amesema kutokana na
mwamko mkubwa iliyonayo Serikali wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kukua na
kufanikiwa katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini, Nemc itajikita katika
kuhakikisha inashirikiana na wizara katika kuhamasisha na kuelimisha wachimbaji
wadogo juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
Aidha, amebainisha
kuwa, kutokana na vigezo vya awali ambavyo viliwafanya wachimbaji wadogo
kutokupewa cheti cha mazingira zitaboreshwa na kuwawezesha kupata cheti hicho.
Amesema, wachimbaji
wadogo watapaswa kusajili miradi yao katika Ofisi za Kanda za Baraza la Hifadi la
Mazingira ambao watakagua miradi hiyo na
baada ya kujiridhisha watawapatia vyeti hivyo.
Waziri wa Madini,
Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Samuel Gwamaka
Mafwenga (kulia) na Meneja wa kanda ya Kati Arnold Mapinduzi (kushoto) mara
baada ya kumaliza mazungumzo mafupi ya namna ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kuhifadhi
mazingira.
No comments:
Post a Comment