Na Asteria Muhozya,
Mbinga
Maafisa Madini nchini
wametakiwa kutobagua migodi midogo kwa kuelekeza nguvu kwenye migodi
mikubwa tu huku wakisisitizwa kutatua migogoro kwenye
maeneo yao ya kazi na kuelezwa kuwa, watakaobainika
wakibagua migodi hiyo na kutotatua migogoro wataondolewa kwenye nafasi zao.
Hayo yalibainishwa
Januari 17 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini
aina ya Sapphire wakati wa ziara yake
katika kijiji cha Masuguru, Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara hiyo
ikilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo pamoja na
kusikiliza kero za wachimbaji katika migodi hiyo, ambapo wachimbaji waliwasilisha kero za kutaka
kutengewa maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji, bei elekezi za madini ikiwemo kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye migodi yao.
Akizungumza kijijini
hapo, alimtaka Afisa Madini mkoa wa Ruvuma hukakikisha anaishughulikia kero
hiyo na kuitatua mara moja na kuongeza
kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano anataka wachimbaji nchini wachimbe madini,
hivyo, maafisa madini kote nchini wahakikishe wanashughulikia kero
katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kusuluhisha migogoro.
“Sisi ni matajiri,
tumebarikiwa madini ya vito. Wachimbaji chimbeni lakini mchimbe katika maeneo
yaliyoruhusiwa kuchimbwa”.alisisitiza.
Alisema kuwa, kama
mgogoro ni mkubwa wapo viongozi wa vyama vya wachimbaji wahakikishe kuwa wanafikisha migororo hiyo na kusema “tuleteeni
na sisi lakini usipoishughulikia
migogoro hiyo tutakuondoa.
Aliongeza kwamba,
serikali inalenga katika kuwatoa wachimbaji wadogo kutoka katika uchimbaji
mdogo kwenda uchimbaji wa kati na
hatimaye mkubwa na ndiyo sababu inaendelea na ujenzi wa vituo vya umahiri katika maeneo mbalimbali nchini ikilenga
katika kutoa elimu ya uchimbaji bora, uchenjuaji bora, biashara ya madini na
ujasiliamali ili kuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo wanakua.
Aliongeza kuwa, elimu
ya ujasiliamali ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa itawaandaa kuwa
na uchimbaji endelevu na wenye tija.
Akijibu ombi la
ruzuku, aliwataka wachimbaji wadogo
kujiunga katika vikundi vidogo vidogo
ili iwe rahisi kwa wachimbaji hao kufikiwa ikiwemo kupatiwa huduma za leseni, elimu,
vifaa, kuwamilikisha, kuwapatia mikopo na kuwafuatilia jambo ambalo litapelekea wafanye kazi kwa
urahisi na kwa kulipa kodi za serikali na wao kubaki na kipato kitakachowezesha maisha bora.
Alisema uwepo wa
mazingira mazuri migodini utasaidia vijana kufanya kazi na hivyo kuwa na taifa
lenye watu wanaofanya kazi. Aliwataka
maafisa madini wote kuhakikisha wanashughulikia migogoro ya wachimbaji wadogo
na kueleza kwamba, endapo serikali itakuta migogogoro ya wachimbaji wadogo katika maeneo yao wataondolewa.
Aliongeza kwamba,
wizara imejipanga na tayari kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya wachimbaji
na kuwasisisitiza kuhakikisha wanauza madini wanayoyachimba katika maeneo rasmi.
Akizungumzia suala la
broker, aliwataka kuhakikisha
wanakuwa na leseni ya kufanya shughuli hizo ikiwemo vifaa vya kupimia madini na
kuwataka kulipa kodi. Pia, aliwatahadharisha wachimbaji wanaoshirikiana na broker wasiokuwa na leseni
kuacha kwani kwa kufanya hivyo ni kwamba kwamba wote wanaliibia taifa.” Maafisa madini
hakikisheni mnawajua ma broker
wote na wawe na leseni na walipe kodi, “
alisisitiza Nyongo.
Akijibu ombi la ruzuku lililowasilishwa kwake, alisema fedha za ruzuku zilizokuwa zikitolewa
awali hazikuwafikia walengwa wote na kueleza kuwa, wapo waliopata ruzuku hizo
lakini hawakuwa wachimbaji na kuongeza kwamba, hivi sasa wizara inaangalia namna
bora ya kuwasaidia wachimbaji.
Kwa upande wake,
Afisa Madini Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya alisema kuwa, mkoa huo tayari umetenga
maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kwamba watashirikiana na wachimbaji
hao ili suala hilo liweze kuwasilishwa
Tume ya Madini kwa ajili ya hatua zaidi.
Awali , kiongozi wa
wachimbaji aliwasilisha ombi kwa Naibu
Waziri la wachimbaji kupatiwa ruzuku. Alisema mkoa huo umebarikiwa madini ya
ujenzi, nishati, viwanda huku eneo la
Masuguru likibariwa madini ya Sapphire. Alisema eneo hilo liliombwa kwa ajjili
ya uchimbaji mdogo lakini mpaka sasa
bado halijatengwa.
Pia, alisema ipo changamoto
ya kukosekana elimu kwa watendaji vijijini ambao wamesababisha mgizo mkubwa wa
kodi kwa wachimbaji.
Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo mwenye sweta (nyekundu) katika picha ya pamoja na baadhi ya
wachimbaji wadogo wa madini ya Sapphire katika kijiji cha Masuguru Wiaya ya
Mbinga mkoa wa Ruvuma
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga
Cosmas Ishenyi akizungumza jambo wakati wa
mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masuguru. Katikati ni Naibu Waziri
wa Madini Stanslaus Nyongo.
|
No comments:
Post a Comment