Na
Samwel Mtuwa, GST
Watalaam wa Taasisi
ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania-GST)
tarehe 10 Oktoba 2018 walikutana na watalaam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya
China (Geological Survey of China-CGS) kwa ajili ya uwasilishaji na upokeaji wa
taarifa ya mradi wa Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo yaani
(Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika kwa ushirikiano
baina ya Serikali ya China na Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa
ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokbeth Myumbilwa alisema kuwa, Utafiti huo
umekusanya taarifa mbalimbali katika upande wa low density na high density
ambapo kwa upande wa low density utafiti ulifanyika katika Mikoa
ya Mbeya na Songwe na high density ulifanyika kwa nchi nzima .
Akizungumzia juu ya
faida zitokanazo na mradi huu wa ushirikiano , Myumbilwa alieleza baadhi ya
malengo ya mradi kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa
taarifa za jiokemia za nchini zitakazo
ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini, upangaji miji ,pamoja na taarifa
hizo kuweza kutumika katika shughuli mbali mbali ndani ya sekta ya killimo na mazingira.
Alisema kuwa, faida
nyingine ni upatikanaji wa taarifa ambazo zitasaidia pia kuanisha aina mbalimbali za
udongo kwa njia ya Ramani yaani (Geochemical Atlas Map of Tanzania).
Mnamo mwaka 2009 serikali
ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Geological Survey zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la
kuanzisha mradi huu wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka
2013mpaka 2018.
Akizungumza wakati wa
kufunga hafla hiyo, Myumbilwa alishukuru kwa
mafanikio makubwa ya mradi huo ,
pamoja ushirikiano mzuri uliokuwepo wakati wa utekelezaji wa mradi toka
ulipoanza mwaka 2013.
Katika hafla hiyo ya upokeaji
wa taarifa GST iliwakilishwa na watalaam 11
na upande wa China CGS uliwakilishwa
na watalaam Sita Sun Xiaoming ambaye ni mkurugenzi wa CGS, Sun Kai , Wang
Huichu , TengXuegian , Li Janjian , Liu Xiaoyangi na Gong Kenghui.
No comments:
Post a Comment