Na
Asteria Muhozya, Songea
Waziri Kairuki
alimweleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, wizara ilitoa maelekezo kwa wahusika kwamba wanatakiwa kuwasilisha barua ya ridhaa ya Waziri wa
Maji, ridhaa ya Wakala wa Barabara nchini (TANROAD), ridhaa ya Bodi ya Bonde la
Mto Ruvuma/Pwani na Kusini ili wizara ijiridhishe kabla ya kutoa maamuzi.
“Tunataka
tujiridhishe na approval kutoka
katika maeneo hayo na vikipatikana vyote, nitafanya uamuzi. Kwa sasa ipo ridhaa
ya bodi ya bonde la mto Ruvuma,” alisisitiza Waziri Kairuki.
Pia, akifafanua kuhusu kusimama kwa shughuli za uchimbaji wa madini
ya Uranium unaofanywa na Kampuni ya
Mantra Tanzania Limited, waziri Kairuki alisema kuwa, kampuni hiyo iliomba kusisitisha shughuli zake
kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na
bei ya madini hayo kushuka katika soko la dunia na kwamba , suala hilo bado
linafanyiwa kazi kitaalam na kiuchumi hivyo, bado serikali haijatoa majibu
kuhusu suala husika.
Kuhusu upatikanaji wa masoko kwa wachimbaji wa
madini, Waziri Kairuki alieleza kuwa, tayari
serikali imepanga kuanzisha masoko ya madini katika maeneo mbalimbali nchini, na hivyo kutoa rai kwa Wakuu wa Mikoa nchini kutenga maeneo kwa ajili
ya uanzishwaji wa masoko hayo. Waziri Kairuki
alitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Christina ambaye alitaka kujua ni namna gani serikali inawasaidia
wachimbaji wadogo kupata masoko ya kuuzia madini madini yao.
“Mhe. Waziri Mkoa
wetu umejaliwa kuwa na madini ya aina mbalimbali na madini haya yamekuwa ni
kichocheo cha uchumi. Sasa, bado wachimbaji wetu wanapata changamoto ya masoko
kwa ajili ya kuuza madini yao,” alisema Mkuu wa Mkoa Mndeme.
Akizungumzia ujenzi wa Vituo vya Umahiri, Waziri Kairuki
alisema, ujenzi wa vituo vya umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali nchini vinagharimu
takribani Bilioni 11 ambao ni mkopo
kutoka Benki ya Dunia. Aliongeza kuwa, Songea ni eneo ambalo serikali inaliangalia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za ukataji na uongezaji
thamani madini.
Alisema kuwa,
serikali iliona umuhimu wa kuwepo na vituo hivyo kutokana na wananchi wengi kutamani kuingia katika shughuli za
uchimbaji lakini bado uchimbaji wao umekuwa si salama na wenye tija
hivyo, uwepo wa kituo hicho utawezesha kutoa elimu ya uchimbaji sahihi na wenye
tija.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Christina Mndeme akizungumzia uwepo wa kituo hicho alisema, kukamilika
kwa kituo hicho kutawezesha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika
mkoani humo, kupanua wigo wa shughuli za uchimbaji na wachimbaji kuchimba kwa
faida.
Aliongeza kwamba,
wachimbaji watapata taarifa sahihi wa mahali gani wauze madini yao na pia uwepo wake utawezesha kutangaza aina ya madini
yanayopatikana mkoani huo.
Vilevile, alisema
kuwa, kituo hicho kitawezesha kupunguza migogoro kati ya wachimbaji wadogo na
wakubwa kwani kitawezesha kupata taarifa sahihi za wapi wachimbe madini.
Naye, Afisa Madini
Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya alisema kuwa, ujenzi wa kituo hicho utawezesha
kurahisisha upatikanaji wa takwimu za madini za mkoa huo, wachimbaji kupata
elimu ya utaalamu wa uchenjuaji bora wa madini, elimu ya ujasiliamali wa
shughuli za madini, afya na usalama mahali pa kazi.
Pia, aliongeza kuwa,
uwepo wa kituo hicho chenye nafasi kubwa, kitaweza kuwahudumia wachimbaji wengi
zaidi.
Waziri Kairuki
alitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Songea Novemba 26.
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Mkuu wa MKoa wa Ruvuma Christina
Mdeme (kulia ) wakichanganya kokoto
katika Kituo ch Umahiri Songea wakati wa
ziara Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Sehemu
ya jengo la Kituo cha Umahiri Songea katika hatua zake za ujenzi
Afisa
Madini Mkazi wa Songea Abraham Nkya akieleza jambo wakati wa ziara ya
Waziri wa Madini Angellah Kairuki alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa
kituo hicho.
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki kushoto) Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdeme (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Songea
Ploliti Mgema wakijadiliana jambo wakati
Waziri Kairuki alipomtembelea Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake.
Baadhi
ya Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea.
Waziri
wa Madini ANgellah Kairuki akiteta jambo na AFisa Madini Mkazi Mkoa wa Ruvuma
Abraham Nkya wakati wa ziara ya Waziri Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Kituo cha Umahiri Songea. Wa Pili Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina
Mdema , Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Madini Gladness Mkambaita na wa kwanza kulia ni
Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, Andrew Eriyo.
No comments:
Post a Comment