Na Greyson Mwase,
Leo tarehe 16
Novemba, 2018 Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) imekutana kwenye Ofisi za
Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma
lengo likiwa ni kupokea na kujadili taarifa za kampuni zilizowasilisha mipango ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya
madini kama sehemu ya maombi ya leseni za madini.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki
(kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume
ya Madini, Profesa Shukrani Manya.
Wajumbe wa Kamati ya
Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini wakifuatilia maelezo yaliyokuwa
yanatolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo
pichani) katika kikao hicho.
Sekretarieti ya kikao
hicho ikinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta
ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki pamoja na wajumbe wengine katika kikao hicho.
Mwakilishi kutoka
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ringo Iringo akichangia jambo kwenye
kikao hicho.
Katibu Mtendaji wa
Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akifafanua jambo katika kikao hicho
No comments:
Post a Comment