Na Rhoda James, Dodoma
Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki ameagiza Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA)
kuhakikisha kuwa wanakuja na Mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji kazi
katika Sekta ya wachimbaji wadogo na kuweka mfumo bora wa kulipa Kodi za
Serikali.
Waziri Kairuki,
ameyasema haya jana tarehe 30 Oktoba, 2018 alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa
Uchanguzi wa Viongozi wa FEMATA
uliofanyika katika Hoteli ya Afrikan Dreams jijini Dodoma.
Kairuki amesema kuwa,
Ukilinganisha wachimbaji wakubwa kwa wadogo nchini, wakubwa ni asilimia nne tu
wakati wachimbaji wadogo ni asilimia 96 lakini ukitazama mchango wao kwa Pato
la Taifa ni kinyume chake.
“Tunataka FEMATA
mshiriki kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanachangia kikamilifu katika Pato
la Taifa,” alisema Kairuki.
Akizungumza katika
Mkutano huo, Kairuki aliwataka wajumbe wote kutumia vyema furasa hiyo katika
kujadili na kupanga mikakati itakayotekelezwa na kuimarisha Vyama vya
wachimbaji wadogo Kimkoa (REMAS), FEMATA na hatimaye kuimarisha wachimbaji
wadogo wa madini nchini.
Aidha, Waziri Kairuki
amewapongeza FEMATA kwa kuandaa mkutano huo na kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara
ya Madini na kuhaidi kuwa atafanya kazi kwa karibu zaidi nao na nimatumaini
yake kuwa ifikapo 2025 Sekta ya Madini itachangia ailimia isiyopungua10
ukilinganisha na mchango wa sasa ambao ni asilimia 4.8 kwa Pato la Taifa.
Akitoa pongezi kwa
Uongozi wa FEMATA, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge alieleza kuwa
ni matumaini yake kuwa wachimbaji na Wafanyabiashara wa madini wataendelea
kulipa kodi zote serikalini kama inavyotakiwa.
Kwa upande wake, Rais
wa Wachimbaji wa madini nchini John Bina amesema kuwa, atasimamia kikamilifu
ulipaji kodi, uchimbaji salama na endelevu kupitia FEMATA.
Waliohudhuria mkutano
huo ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Manaibu mawaziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko, Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge,
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Viongozi mbalimbali kutoka
Serikalini ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira (NEMC),
Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA), Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Benki Kuu (BOT) pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji na
Wafanyabiashara wa madini.
Rais mteule wa FEMATA John Bina
akihutubia Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini mbalimbali (hawapo pichani)
jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA jijini
Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA
uliofanyika tarehe 30 Oktoba, 2018 jijini Dodoma.
Wachimbaji wa Madini na wafanyabiashara
wa madini wakiwa katika Mkutano Mkuu wa FEMATA uliofanyika katika hoteli ya
African Dreams jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
akihutubia Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini mbalimbali (hawapo pichani)
jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA jijini
Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith
Mahenge akihutubia Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini mbalimbali (hawapo
pichani) jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA
jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
No comments:
Post a Comment