Nuru Mwasampeta,
Pwani
Naibu Waziri wa Madini
Doto Biteko amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kushirikiana
na kampuni ya Rack Kaloin inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya kaolin
wilayani humo kwani imeonesha uzalendo kwa kulipa mirabaha ya serikali inavyopaswa
pamojana kuwa na ushirikiano mzuri na jamii inayouzunguka mgodi huo sawasawa na
taratibu na sheria ya madini inavyoeleza.
Ametoawito huo tarehe
22 mwezi Oktoba alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani wilayani Kisarawe
baada ya kutembelea eneo la machimbo ya mgodi huo na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Adam Ng’imba.
Akielezea dhumuni la ziara
hiyo, Biteko alisema ni kukagua shughuli za uchimbaji zinazoendelea pamojana kujiridhisha
na suala zima la utunzwaji wa kumbukumbu za uchimbaji nauuzwaji wa madini hayo utakaopelekea
Serikali kulipwa kodi stahiki inayotoka na na faida inayopatikana kutokana na uchimbaji
na biashara ya madini.
Akizungumzia suala zima
la ulipwaji wa mirabaha ya uchimbaji, Biteko alisema mwekezaji anapaswa kulipa kodi
hiyo kutokana na kiasi alichokiuza kwenye soko hiyo ikiwa ni pamoja na gharama za
usafirishaji kutoka sehemu za machimbo mpaka soko lilipo.
Amesema, awali wawekezaji
wa madini walikuwa wakilipa mrabaha kwa gharama ya eneo la machimbo ambapo madini
hayo yanaposafirishwa ndipo dhamani yake inaongezeka na kuuzwa kwa gharama ya juu
hivyo walikuwa wakiibia Serikali kiasi kikubwa cha pesa.
Aidha, Biteko amekiri
kuwa jukumu la kutoa elimu kwa wawekezaji wasiojua taratibu na sheria za kufanya
biashara hiyo ni yake baada ya mnunuzi wa madini hayo kubainika kutokuwa na elimu
ya kutosha ya kufanya biashara hiyo. “Najua hujui taratibu za kufanya biashara hii,
nitakuelimisha kwani hili ni moja kati ya majukumu yangu” alisema.
Akielezea moja ya taratibu
anazopaswa kuzifuata mchimbaji au msafirishaji wa madini, Biteko alisema anapaswa
kuwa na aidha leseni ya uuzaji wa madini (Dealer licence) au kuwa na leseni ya uchimbaji
au zote mbili kwa pamoja.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rack Kaloin alisema wanaendelea vizuri na kazi
za kila siku na kwamba watafanya mazungumzo na wanakijiji ili kuona namna watakavyonufaika
moja kwa moja kutokana na uchimbaji huo baada ya kupeleka pesa serikali zamita aambazo
matokeo yake kwa wanakijiji wanaozunguka mgodi huo hayaonekani.
Kwa upande wake
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwambapa amemshukuru Biteko kwa kutembelea
Wilaya hiyo na kwa maelekezo aliyoyatoa na kuahidi kuwa halmashauri yake itaendelea
kushughulikia changamoto mbalimbali za sekta ya madini ili waweze kuwa na uzalishaji
mzuri na wenye tija kwa wawekezaji na serikali kwa ujumla.
Akikamilisha ziara hiyo
Biteko alitoa wito kwa wachimbaji wadogo na wanakisarawe kwa kusema waendelee kushirikiana
na ofisi za madini kwani kazi ya Serikali ni kuwafanya wachimbaji hao kukua na kuwa
na uchmbaji wenye tija. “Kazi yetu sisi kazi yetu ni kuwalea wao waweze kuchimba
kwa kufuata sheria lakini zaidi sana kuwafanya wawe wachimbaji wanaokua kutoka uchimbaji
mdogo, wa kati na baadaye kuwa wachimbaji wakubwa.”
Aidha, alitoa wito kwa
halmashauri ya Kisarawe kisarawe kuwapa ushirikiano wa kutosha wachimbaji na kwamba
wawalee na wao kwani hakuna sababu yoyote ya kuwa na migogoro kila mahali lakini
pia wachimbaji wasiwanyonge wala kuwanyonya wanakisarawe isipokuwa wazingatie taratibu
zilizowekwa.
No comments:
Post a Comment