Na Nuru Mwasampeta,
Naibu Waziri wa
Madini Doto Biteko amezitaka halmashauri za wilaya kufanya kazi na wizara ili
kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao kabla
hazijasababisha madhara makubwa kwa jamii.
Aliyasema hayo
mwanzoni mwa wiki alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani wilaya ya
Mkuranga alipofika ili kukagua shughuli za uchimbaji wa mchanga unavyoendelea
pamoja na kukagua namna ya ulipwaji wa mirabaha ya Serikali inavyofanyika.
Akizungumza katika
kikao baina yake na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Hassan Sanga, Biteko
alisema “Sisi ni wamoja hivyo tufanye kazi kwa pamoja, tunajifunza pamoja ili
tuamue kwa pamoja”.
“Tunatamani mambo
mengi yaishie huku chini lakini endapo kuna masuala yanahitaji msukumo wa
wizara ninyi mtueleze” alisistiza Biteko.
Aidha, Biteko
aliwataka viongozi wa wilaya ya Mkuranga kuhakikisha tozo zinazotozwa na
halmashauri hiyo ziwe ni zile zinazokubalika kisheria ili kupunguza migogoro
midogomidogo baina ya Serikali na wachimbaji lakini pia kuwasaidia wachimbaji ili
waweze kukua na kuongeza kipato chao.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga alibainisha uwepo wa utoaji wa leseni bila ofisi yake kushirikishwa
na hivyo kuwawia ugumu pindi wanapotakiwa kuchukua hatua za kuzuia eneo husika
kufanyika shughuli za uchimbaji. “Mchanga unachimbwa kiholela ukiuliza wanasema
wanavibali kutoka wizara ya ardhi, madini lakini pia wana vibali kutoka Nemc,
tunashindwa kuwachukulia hatua.
Akizungumzia suala
hilo Biteko alisema, mmiliki yeyote wa leseni ya madini hatakiwi kuanza kazi pasipo
kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ambaye atapaswa kukutambulisha katia ngazi
zote mpaka katika uongozi wa kijiji leseni yako.
Aidha aibainisha kuwa
maeneo ya jeshi, vyanzo vya maji, maeneo ya hifadhi hayaruhusiwi kutolewa
leseni lakini pia aliwataka viongozi hao wa wilaya kusema maeneo wanayodhani
hayapaswi kutolewa leseni na kwamba wizara itatii kwa kutokutoa leseni kwa
maeneo hayo.
Pia alielezea mamlaka
ya wilaya kuwa inauwezo wa kuomba leseni zote zilizoombwa kwa kipindi Fulani
ili kujiridhisha kama maeneo hayo yanaweza endeleza shughuli za uchimbaji na
kama ni vinginevyo leseni zinafutwa.
Pamoja na hayo,
Biteko aliutaka uongozi wa wilaya kuwalea
wachimbaji na kuondokana na urasimu usiokuwa na sababu, “tuwahurumie
watu, Urasimu usiokuwa na sababu sisi wizara ya madini tunasema hapana.”
Alisema Biteko.
Biteko alitanaibisha
kuwa, wawekezaji wanatumia pesa nyingi kuwekeza kwenye uchimbaji na wengine
wana mikopo katika mabenki hawalali vizuri hivyo tuwasaidie ili waweze kufanya
kazi zao kwa utulivu na kupata kile wanachotarajia.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika wilaya hiyo kulia kwake ni
Mkuu wa Wilaya hiyo Filberto Hassan Sanga.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko akitembea kuelekea eneo ambako uchimbaji wa
mchanga unafanyika.
|
Mmoja
wa wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa mchanga katika kijiji cha Mwanandilati
akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (Hayupo pichani)
|
No comments:
Post a Comment