Wednesday, October 10, 2018

Wizara ya Madini yangaa’ra katika Maonesho ya Madini ya dhahabu Mkoani Geita


Na Rhoda James,

Wizara ya Madini imekuwa mshindi wa kwanza katika taasisi za Serikali zilizoshiriki Maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya dhahabu mkoani Geita yaliyoanza tarehe 24 - 30 Septemba, 2018.

Maonesho hayo yaliyofana, yaliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan trade).

Maonesho hayo yaliyoshirikisha makampuni 250 kutoka maeneo mbalimbali nchini yalishirikisha wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.

Aidha, Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka mkoani Geita na yatakuwa yanaandaliwa kwa kushirikiana na taasisi hiyo ya  Tan trade.

Imeelezwa kuwa Maonesho yajayo yataboreshwa zaidi na yatashirikisha mataifa mbalimbali na Wizara ya Madini itashiriki kuyatangaza ili wadau wengi zaidi waweze kushiriki.


Cheti cha ushidi cha ambacho Wizara ya Madini imepata  katika Maonesho ya Madini mkoani Geita. (hayupo pichani.) 

Muonekano wa kikombe ambacho Wizara imekipata katika Maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya dhahabu mkoani Geita yaliyoanza tarehe 24 - 30 Septemba, 2018. 

Mjiologia kutoka Wizara ya Madini, Joseph Ngurumwa (mwenye shati la bluu) akiwa pamoja na Mjiolojia kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Priscus Kaspana.

No comments:

Post a Comment