- Ni baada ya waziri Kairuki kubaini madudu baada ya ziara ya kushtukiza
Waziri wa Madini Mhe.
Angellah Kairuki ameyafungia maduka manne ya vito na usonara yaliyopo katika
Mtaa wa Indiragadhi baada ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za
uuzwaji wa madini hayo.
Hayo yamebainika mara
baada ya Kairuki kufanya ziara ya kushtukiza ya kukagua na kujiridhisha endapo
wafanyabiashara hao wanafuata taratibu na shaeria za kufanya biashara ya madini
Jijini Dar es Salaam na kubaini wengi wao kuzikiuka na kuisababishia Serikali
kutokupata mapato halali ya mrabaha kutoka kwa wauzaji wa madini hayo.
Maduka yaliyofungiwa
wakati wa ziara hiyo ni Sami Jewellers, New Gold Point, Almasi Jewellers pamoja
na Queens Jewellers ambapo wafanyakazi wake hawakutaka kumtaja mmiliki wa
maduka hayo yanayodaiwa kuwa ni ya mtu mmoja.
Waziri Kairuki
alibainisha kutoridhishwa na wafanyabiashara wa madini hao mara baada ya
kumaliza ziara yake ya siku ya kwanza na hivyo kuagiza maduka hayo kufungwa. “Baada
ya kufanya ziara hii na kujionea madudu yanayoendelea nimeelekeza kufungwa kwa
maduka manne kutokana na mmiliki wake kutokuzingatia utuzwaji wa kumbukumbu na
kufanya biashara hii bila kuwa na leseni kutoka wizara ya Madini kama sheria zinavyoelekeza”.
Alisema.
Alikazia kuwa, ili
kufanya biashara hii, mfanyabiashara anapaswa kuwa na leseni mbili ambapo moja
inatolewa na Wizara ya Madini na nyingine inatolewa na Wizara ya Viwanda
Biashara na Uwekezaji.
Aidha, Waziri Kairuki
alibaini kuwa, Wafanyabiashara hao wanakiuka au hawafuati mfumo elekezi wa
utunzwaji wa kumbukumbu za mauzo na manunuzi ya madini hayo kutokana na maduka
yote aliyoyatembelea kutokufuata utaratibu halali wa kutunza kumbukumbu hizo.
Kutokana na
kutoridhishwa na ujazwaji wa kumbkumbu hizo Waziri Kairuki aliwaagiza
wafanyabiashara hao kuhkikisha wanzingatia namna elekezi ya kutunza taarifa
hizo ili kujiweka katika hali salama pindi itakapobainika kuwa madini
wanayouziwa ni ya wizi au vinginevyo.
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyeamua kuambatana na Waziri kwenye ziara yake ya
siku ya kwanza alisema amesikitishwa sana kuona katika mkoa wake bado kuna watu
wanaokiuka sharia na taratibu za nchi na kueleza kuwa wasipotaka kufuata sharia
kwa hiari basi sharia zenyewe zitawalazimisha wazifuate.
“Mimi kama Mkuu wa
Mkoa huu najisikia vibaya kuwa na wafanyabiashara ambao wanakiuka taratibu na
kuwa wajanja wajanja wakati wanafahamu msimamo wa Serikali ya awamu ya tano
kuwa ni wajibu wa kila mmoja kufuata sharia na taratibu za ulipwaji wa kodi”.
Alisisitiza.
Aidha, Makonda
amewataka wafanyabiashara katika mkoa wake kuweka mazingira yao ya biashara
vizuri ili kuepuka usumbufu watakaoupata endapo watakiuka taratibu hizo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kwanza kulia akifuatiwa na Waziri wa Nishati mara
baada ya kuwasili katika mtaa wa Indiragadhi kwa ziara ya ukaguzi wa maduka ya
madini na usonara ili kujiridhisha endapo wafanyabiashara hao wanafuata
taratibu za kufanya biashara hiyo.
|
Waziri
wa Madini Mhe. Angellah Kairuki mwenye blauzi ya mistari akimsikiliza mwalimu
wa ukataji vito Farai Runyanga (kushoto kwa Waziri) kutoka nchini Zimbambwe
aliyefika kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wazawa ili kujishughulisha na kazi
hiyo ya kusanifu madini nchini.
|
Waziri
wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akiendelea na ukaguzi wa taarifa za mauzo wa Madini.
|
No comments:
Post a Comment