Na
Asteria Muhozya, Morogoro
Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo amewataka Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini
kuhakikisha kwamba wizara hiyo haipati hoja kutokana na kukikukwa kwa taratibu
za manunuzi baada ya wajumbe hao kupatiwa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za
Manunuzi ya Umma.
Pia, wajumbe hao wametakiwa kuhakikisha wanafamu kwa
weledi Sheria na Kanuni za manunuzi
ili waweze kutoa maamuzi sahihi.
Naibu Waziri Nyongo
aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika ofisi za Madini Mkoa
Morogoro tarehe 21 Septemba,2018.
Naibu Waziri Nyongo
alisema hitaji la kuwapatia mafunzo wajumbe hao linafuatia upya wa wizara hiyo
ikiwemo wajumbe wa bodi hiyo ambao wengine wametoka katika sekta mbalimbali
hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi zilizoanishwa.
“Masuala ya manunuzi
yanalalamikiwa sana kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi. Lakini pia, manunuzi
ya umma yamekuwa na matatizo kutokana na kuwepo Mikataba mibovu kwa hiyo baada
ya ninyi kupatiwa mafunzo haya, sitarajii vitu kama hivi kujitokeza.
Pia, Naibu Waziri
Nyongo aliwataka wajumbe wa bodi kuhakikisha kuwa, mafunzo waliyoyapata
yanawasaidia kuepukana na vitendo vya rushwa wakati wa kusimamia shughuli za
manunuzi ya wizara.
“Ukiiba mali ya umma
kuna siku wengine watakuja na watahoji. Siku zote mali ya umma ni ya kuogopa,”
alisisitiza Naibu Waziri nyongo.
Naye, Mwenyekiti wa
Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Utawala na RasilimaliWatu Wizara ya Madini, Issa Nchasi, alisema kuwa, wakati wa mafunzo wajumbe hao
walipata nafasi ya kujifunza kuhusu Sheria, Mikataba na Kanuni za Manunuzi
ikiwemo kupata uzoefu wa shughuli za manunuzi na namna zinavyofanyika.
Akizungumzia manufaa
ya mafunzo, Nchasi alisema kuwa yamekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa
yatawawezesha wajumbe kutoa maamuzi
sahihi ikiwemo kumshauri Afisa Masuhuli kufuata Sheria na Kanuni ili kuepuka
ununuzi ambao hauzingatii sheria.
Aliongeza kuwa, mafunzo
hayo yalilenga kuwawezesha wajumbe kuelewa Sheria ili kufanya kazi zao kwa
weledi.
Kwa upande wake,
Mkufunzi kutoka Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA),
Paschal Komba aliipongeza wizara ya Madini kwa kutoa mafunzo hayo kwa wajumbe
wa bodi hiyo na kuelea kuwa, yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia Sheria na taratibu za ununuzi wa umma.
Mafunzo hayo
yalitolewa na Wataalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
![]() |
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya
masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini
wakikabidhi
![]() |
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya
masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini
wakikabidhi
![]() |
Baadhi
ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakiwa wakijadiliana wakati wa mafunzo kuhusu masuala
ya manunuzi kwa wizara hiyo
![]() |
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijadiiana jambo na Wajumbe wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni na Mkurugenzi w
Utawala na RasilimaliWatu Issa Nchasi na Mjumbe wa Bodi na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Athony Tarimo.
Wengine ni Maafisa kutoka PPRA waliotoa mafunzo hayo
![]() |
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya
masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini
wakikabidhi
![]() |
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya
masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini
wakikabidhi
No comments:
Post a Comment