Na Rhoda James, Geita
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka Mgodi wa Geita Gold Mine Ltd
kuwalipa fidia wananchi waliopata madhara ya nyufa katika katika nyumba zao kutokana
na shughuli za uchimbaji wa madini wa kampuni hiyo.
Naibu
Waziri Nyongo aliyasema hayo tarehe 26 Septemba, 2018 wakati alipofungua
Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu
mkoani Geita kwa niaba ya Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
Alitoa
rai kwa Wachimbaji wadogo wa madini kote nchini kushiriki maonesho hayo
yanayoendelea mkoani humo kwa kuwa yatawanufaisha kwa kupata fursa ya kujifunza
kuhusu teknolojia mbalimbali na namna bora ya uchimbaji, uchenjuaji, ikiwemo
kupata elimu ya kulinda mazingira na kuzalisha kwa tija.
Pia,
aliwataka Wakuu wa mikoa yote nchini pamoja na Wakuu wa wilaya zote kujifunza
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi ili kuhakikisha kuwa wananchi
wao wanafaidika na rasilimali pamoja na mazao yanayolimwa katika maeneo yao.
“Mkifanya
maonesho ya aina hii katika mikoa yenu kulingana na mazao au rasilimali mlizonazo
katika mikoa yenu wananchi wenu watafaidika,” alisema Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo.
Vilevile,
Naibu Waziri Nyongo, aliwataka wananchi wa mkoa wa Geita na Kagera pamoja na wadau wa
madini ya dhahabu kujipanga ili kuhakikisha kuwa maonesho hayo yanafanyika kila
mwaka.
Pia,
Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na
uongozi kutoka Mkoa wa Geita kuhakikisha kuwa wanayatangaza maonesho hayo kwa
kiasi kikubwa ili yaweze kufahamika duniani kote hatimaye wadau wa madini
waweze washiriki kwa wingi.
“Wateja
wengi wa madini wanatoka nje ya nchi na ni vyema pia wakajua chanjo cha madini
hayo kiko wapi,” alisema Nyongo.
Akizungumzia
mchango wa Sekta ya madini katika pato la taifa, Naibu Waziri Nyongo alisema
kuwa, mchango wa Sekta ya Madini bado ni kidogo na kuongeza kuwa, malengo ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa, mchango wake unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka
2025.
“Mwaka
2016 na 2017 sekta ya madini imechangia kwenye pato la taifa asilimia 4.8
lakini tunatarajia ifikapo 2025 sekta ya madini itachangia zaidi ya asilimia10,”
alisema Nyongo.
Wakati
huo huo, Naibu Waziri Nyongo ametoa onyo kwa wachimbaji wadogo kuachana na
tabia ya kutorosha madini na kueleza kuwa, atakayekamatwa akifanya hivyo
atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia,
Naibu Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Geita na wadau
mbalimbali akiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Bishara Tanzania (TanTrade) pamoja
na Wizara ya Madini kwa kuandaa maonesho ya madini ya dhahabu mkoani Geita.
Pia,
amewapongeza umoja wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu (GEREMA) kwa
kuhakikisha kuwa Maonesho hayo yanafanyika kama ilivyokusudiwa.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi alisema kuwa, ni matarajio
yake kuwa maonesho hayo yatakuwa ya kitaifa na hatimaye ya dunia nzima na
kuongeza kuwa, anataka maonesho hayo ya madini ya dhahabu kufanyika kila mwaka
mkoani kwake.
Pia,
alisema alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya madini kwa ushirikiano
inayotoa kwa wachimbaji wadogo kupitia taasisi za GST na STAMICO.
Vipande vitatu vya madini katika gram tofauti baada ya kuzalishwa
na kampuni ya Wachimbaji Wadogo mkoani Geita.
|
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwahutubia wananchi wa Mikoa ya Geita na
Kagera tarehe 26 Septemba, 2018 katika Viwanja vya Kalangalala mkoani Geita.
|
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Luhumbi akiwahutubia wananchi wa Geita na
Kagera na wadau wa madini katika maonesho ya Madini ya dhahabu mkoani Geita.
|
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akisalimiana na wananchi wa
Geita pamoja na wananchi wa mkoa Kagera katika Viwanja vya CCM Kalangalala
mkoani Geita.
|
Mkuu
wa Wilaya ya Ilamba, Emmanuel Luhahula
aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Singida akisalimia wananchi wa mikoa ya Geita
na Kagera katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.
|
Mwenyekiti
wa Wachimbaji Wadogo Geita (TCCIA), Chacha Mwita akisalimia wananchi wa Geita
na Wadau wa madini ya dhahabu mkoani Geita
|
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni katika banda la
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) alipowatembelea katika Viwanja vya CCM
Kalangalala mkoani Geita.
|
No comments:
Post a Comment