Na Asteria Muhozya,
Wizara ya
Madini imeanza kukutana na Kamati Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia
leo tarehe 29 Oktoba hadi Novemba 1, 2018.
Katika
kikao cha leo Wizara imewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya
Maendeleo.
Akiwasilisha
Taarifa kuhusu Ujenzi wa Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa, Kaimu Mkurugenzi wa
Sera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal amesema hadi kufikia mwezi
Septemba,2018, kazi ya ujenzi wa mgodi na usimikaji wa mitambo ya uchenjuaji
imekamilika kwa asilimia 80.
Kuhusu
mradi wa One Stop Center, eneo la Mirerani, amesema uko kwenye maandalizi ya
kuanza ujenzi na kuongeza kuwa, jengo hilo litakapokamilika
litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo huduma za Utoaji na Usimamizi
wa Leseni za Madini, Uhifadhi wa madini kwa usalama , Kodi na tozo
mbalimbali ikiwemo ofisi za TRA, Huduma za kifedha, ikiwemo Benki na Ofisi za
Benki kuu, Hud za tathmini na uthamini madini, Ofisi za Madini na Chumba maalum
cha kufanyia minada ya madini.
No comments:
Post a Comment