Na
Nuru Mwasampeta, Dodoma
Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki leo tarehe 28 Septemba, 2018, amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho
la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina ambaye aliambatana na
Mtendaji Mkuu wa Shirikisho hilo, Bwana Haroun Kinega, ofisini kwake jijini
Dodoma.
Katika kikao hicho,
Waziri Kairuki amewashukuru wajumbe hao kwa kumtembelea ofisini kwake na
kujadiliana masuala mbalimbali katika sekta ya madini kwa lengo la kuboresha utendaji
katika sekta ya madini, uchimbaji na wachimbaji wadogo kwa ujumla.
Aidha, Waziri Kairuki
amewataka watanzania wenye mawazo chanya ya kukuza sekta ya madini kutosita
kufika na kutoa maoni yao ili Serikali iweze kuyafanyia kazi ili kuboresha
sekta hiyo kwa manufaa ya jamii nzima ya watanzania na hivyo kuifanya sekta
kuchangia zaidi katika pato la taifa, ajira na kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumzia lengo la
kufika wizarani hapo, Rais wa FEMATA, John Bina amesema ni kujadili kuhusu mafanikio,
changamoto, fursa za wachimbaji wadogo zilizopo katika sekta husika pamoja na
kujadili namna ya kuendeleza sekta ya uchimbaji mdogo wa madini nchini ikiwa ni
pamoja na namna ya kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.
![]() |
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (Katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa
Madini John W. Bina (Kulia) na kushoto kwa waziri ni Mtendaji Mkuu wa
Shirikisho la Wachimbaji wadogo Haroun
![]() |
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA)
John W. Bina alipomtembelea ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment