Na Greyson Mwase,
Leo tarehe 20
Septemba, 2018 mjini Musoma mkoani Mara, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wamekutana na
Wakuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Mara, Watendaji kutoka
Wizara ya Madini kwa ajili ya kujadili taarifa iliyowasilishwa na Kamati
iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza matumizi ya mfuko wa North Mara Trust Fund
kabla ya kutoa maelekezo ya Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Adam Malima (kushoto) akifafanua jambo katika kikao kwa ajili ya kujadili taarifa iliyowasilishwa na kamati
iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza matumzi ya fedha katika mfuko wa North Mara
Trust Fund. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko.
|
No comments:
Post a Comment