Na Greyson Mwase,
Tarehe 19 Oktoba,
2018 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alifanya ziara katika Mgodi wa
Makaa ya Mawe wa Kabulo (Kabulo Coal Mine) uliopo katika eneo la Kabulo lililopo
katika wilaya Songwe mkoani Songwe na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira (Kiwira
Coal Mine) iliopo katika Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya. Mara baada ya kufanya
ziara katika migodi husika, alizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Makaa ya
Mawe wa Kiwira lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili.
Akizungumza katika
mkutano wa wafanyakazi alisema kuwa, kwa sasa Serikali imetenga fedha kwa ajili
ya ukarabati wa barabara ya kutoka Kabulo hadi Kiwira itakayotumika kwa ajili
ya usafirishaji wa makaa ya mawe pamoja na kuhakikisha inalipa stahili za
wafanyakazi mara baada ya taratibu kukamilika. Katika hatua nyingine, Nyongo
aliwataka watumishi kufanya kazi kwa ubunifu na kusisitiza kuwa Wizara ya
Madini itahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.
Wafanyakazi wa Mgodi
wa Kiwira walimpongeza Naibu Waziri Nyongo kwa kazi kubwa ya kusikiliza na
kutatua kero za wachimbaji wa madini nchini pamoja na Taasisi zilizopo chini ya
Wizara.
Meneja Migodi kutoka
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Alphonce
Bikulamchi (katikati) akielezea shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe zinavyofanyika katika Mgodi
wa Makaa ya Mawe wa Kabulo uliopo katika mkoa wa Songwe kwa Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto)
Kaimu Meneja Mkuu wa
Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira uliopo katika wilaya ya Ileje Mkoani
Mbeya, Samwel Kibaranga (kushoto)
akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) reli
inayotumika kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe (haionekani pichani)
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto mbele) akitoa maelekezo katika eneo
la Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Kiwira
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (wa tano kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja
na wafanyakazi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira mara baada ya kumalizika kwa
mkutano
No comments:
Post a Comment