Na Asteria
Muhozya,
Kuanzia tarehe 21, 23 na 24
Agosti, Wizara ya Madini ilikutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini ambapo taarifa mbalimbali za Utekelezaji wa Majukumu na
Miradi zimewasilishwa.
Baadhi ya taarifa zilizowasilishwa katika vikao hivyo ni pamoja
na Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Madini kuanzia mwezi Aprili
hadi Julai,2018, Taarifa kuhusu Uendelezaji na Uwekezaji katika Madini Mkakati na Taarifa kuhusu Uendelezaji ya Migodi ya Makaa ya Mawe.
Aidha, katika vikao hivyo, Kamati ilitoa maagizo
mbalimbali yanayopaswa kufanyiwa kazi na Wizara ili kuboresha Sekta ya Madini
nchini.
* ALICHOKISEMA WAZIRI WA MADINI ANGELLAH KAIRUKI
# Graphite ni madini ambayo tunayapa kipaumbele. Ninawaomba
wananchi na ninyi Waheshimiwa Wabunge mtusaidie kuwaambia wananchi wasikwamishe
miradi ya uwekezaji.
# Tutakapokuwa katika hatua za uchimbaji wa madini ya Urani,
tutakuwa karibu sana na kila hatua itakayofanyika kuhakikisha kwamba hakuna
athari zozote za kijamii. Serikali haitaweka maslahi ya kiuchumi mbele kuliko
ya kijamii.
# Tutafanya Jukwaa kubwa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini
mwaka 2019. Lengo ni kuvutia Wawekezaji na kuwakutanisha wachimbaji na Wabia
lakini pia Taasisi za Kifedha.
*ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI, DOTO BITEKO
# Wachimbaji wetu wanahitaji huduma za umeme, maji na barabara
katika maeneo yao. Yapo baadhi ya maeneo ambayo tayari Mhe.
Waziri amewasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya masuala hayo.
* ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS NYONGO
# Tuna madini mengi ya Kimkakati. Tunaangalia madini
ambayo yatasaidia kusukuma mbele Sekta ya Viwanda.
* ALICHOKISEMA KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI, PROF. SIMON
MSANJILA
# Kama Wizara tunayo nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa
madini. Tunaangalia mfumo mzuri wa namna ya kuwasaidia. Tutawashirikisha
Waheshimiwa Wabunge kuhusu namna ya kufanya jambo hilo kwa ubora zaidi.
No comments:
Post a Comment