Na
Asteria Muhozya,
Waziri wa Madini
Angellah Kairuki, akiongozana na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Longido pamoja na ujumbe aliombata nao wakati wa ziara yake mkoani Arusha, tarehe
9 Agosti,2018, alitembelea eneo la Mpaka wa Namanga, linalotenganisha nchi ya
Tanzania na Kenya.
Waziri Kairuki
alitembelea eneo husika kwa lengo la kukagua na kuangalia namna shughuli za udhibiti
wa utoroshaji wa madini maeneo ya mipakani
zinavyoendelea.
Waziri Kairuki alisema
baada ya kufika eneo husika alikuta kuna suala la changamoto ya upungufu wa
wafanyakazi na hivyo kuahidi kulifanyia kazi kwa haraka suala hilo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo alisema changamoto katika eneo hilo ni upungufu wa
wafanyakazi na kuongeza kuwa, tayari Waziri wa madini ameahidi kulifanyia kazi
suala husika ili kudhibiti utoroshaji madini katika maeneo ya mipaka.
Aliongeza kuwa,
tayari Serikali ya Wilaya imeanza kuweka alama kujua mipaka ya Tanzania katika
eneo husika ikiwemo kufuatilia njia za panya ambazo zinaweza kutumika kutorosha
madini nje ya nchi.
Naye Mkaguzi wa
Migodi, Anold Kisheshi alisema kuwa, serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali
kudhibiti utoroshaji wa madini katika maeneo ya mipaka.
![]() |
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Anorld
Kisheshi wakati akitoa ufafanuzi wa namna scanner katika eneo hilo zinavyofanya
kazi.
|
![]() |
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki akipata maeneo mbalimbali katika eneo Namanga katika
mpaka wa Tanzania na Kenya.
|
![]() |
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Anorld
Kisheshi wakati akitoa ufafanuzi wa namna scanner katika eneo hilo zinavyofanya
kazi.
|
No comments:
Post a Comment