Na Asteria Muhozya,
Longido
Serikali imesema
itatoa Hati za Makosa kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji madini ambao
hawajaendeleza maeneo yao na endapo hawatatii matakwa ya Sheria, watafutiwa
leseni zao na maeneo yao kupewa wombaji
wengine.
Hayo yalielezwa na
Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe 9 Agosti, katika mkutano wa hadhara
wakati wa ziara yake alipotembelea machimbo ya Ruby katika Kijiji cha
Mundarara, Kata ya Mundarara, Wilaya ya Simanjiro mkoani Arusha.
Waziri Kairuki
alitembelea migodi inayochimba madini ya Ruby katika eneo la Mundarara ili kuna
namna shughuli za uchimbaji wa madini
hayo zinavyofanyika ikiwemo masuala ya afya na usalama migodini, kusikiliza
changamoto na migogoro iliyopo katika machimbo hayo.
Alisema kuwa,
Serikali inawajali wachimbaji wadogo nchini na kuwataka wenye nia ya kumiliki
leseni za madini kufika katika ofisi za madini kwa ajili ya kupata taratibu za
uombaji na taratibu nyingine za umiliki
wa leseni na kuongeza kuwa, bado serikali inaendelea kutenga maeneo kwa ajili
ya wachimbaji wadogo nchini.
Akizungumzia suala la
utoaji ruzuku, Waziri Kairuki alimsema serikali inaangalia mfumo bora ambao
inaweza kuutumia katika kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini na kueleza kuwa,
ruzuku hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa
vifaa ama namna nyingine.
Pia, Waziri Kairuki
aliwakumbusha wamiliki wa leseni za madini kuhakikisha wanajitambulisha katika
ofisi za vijiji mahali yalipo maeneo yao
kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji madini ili kutambuliwa na uogozi wa kijiji jambo ambalo litasaidia kuondoa migogoro.
Vilevile, Waziri
Kairuki aliwataka wamiliki wa leseni za madini kuandaa Mpango wa Uwajibikaji
kwa jamii na kueleza kuwa, kwa mujibu wa
sheria ya madini, mwekezaji anapaswa kushauriana na wananchi wa eneo husika, chini ya usimamizi wa
Halmashauri kuhusu maeneo ya uwajibikaji katika uwekezaji wake.
Pia, alizungumzia
suala la Mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi huku akisisitiza kuwa, endapo
kuna shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wananchi katika eneo husika, ni
muhimu jambo husika lifanyike hivyo.
Akitolea ufafanuzi
suala la uongeaji thamani madini, alisema kuwa, serikali imekataza kusafirisha
madini ghafi nje ya nchi ili yaongezewe thamani nchini na kueleza kuwa, tayari
imeandaa mwongozo wa kutafsiri dhana
nzima ya uongezaji thamani madini na baada ya muda mfupi ujao itazungumzia
kuhusu jambo hilo.
Waziri Kairuki alitoa
ufafanuzi huo, baada ya wawekezaji
katika machimbo ya Ruby mundarara kuwasilisha ombi la kutaka madini hayo
yasifirishwe yakiwa ghafi kutokana na aina ya madini yenyewe.
Pia, Waziri Kairuki
alisema kuwa,Wizara kupitia Tume ya Madini itakuwa ikitoa bei elekezi za madini
kila mwezi na kusimamia suala la uendeshaji wa minada ya madini nchini.
Aidh, masuala mengine aliyoyasisitiza Waziri
Kairuki katika mkutano huo ni pamoja wachimbaji kuzingatia Sheria, Kanuni na
Taratibu. Wachimbaji kutunza kumbukumbu za uzalishaji na kuwa wazalendo kwa
kutoa taarifa za wanaotorosha madini nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano huo, alimtaka Waziri
kupitia wizara yake kutoa ufafanuzi wa Sheria ya madini ili kuwawezesha
wachimbaji kuitekeleza kwa mujibu wa kanuni na taratibu zake.
Pia, alimtaka Waziri
wa Madini kusaidia kuweka mfumo mzuri wa biashara ya madini hayo na kuongeza
kuwa, endapo kutawekwa mazingira mazuri ya biashara ya madini hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa
wananchi wa eneo husika, wilaya na hatimaye taifa.
Awali, akisoma risala
ya kijiji, katika mkutano huo, Diwani wa Kata
Mundarara, Alais Mushao aliwasilisha changamoto ya soko la kuuzia madini
ya ruby na kumuomba Waziri asaidie kuhakikisha kuwa, wawekezaji wadogo kupewa
fursa sawa.
Katika mkutano huo,
ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya
ya Longido Frank Mwaisumbe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya , Wataalam
kutoka Wizara ya Madini na Ofisi za Madini.
![]() |
Waziri wa Madini
Angellah Kairuki ( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia)
wakiangalia madini ya Ruby walipotembelea mgodi wa Mundarara Mine uliopo katika
kijiji cha Mundarara , Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, wakati wa ziara ya
Waziri Kairuki katika machimbo hayo.
![]() |
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiangalia namna madini ya Ruby yanavyokatwa
kuondolewa katika miamba walipotembelea mgodi wa Mundarara Mine wakati wa ziara
ya Waziri wa Madini Angellah Kairuki mgodini hapo. Kushoto anayefuatilia ni
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi David Mulabwa.
![]() |
Afisa
Madini akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki maumbile ya miamba katika
migodi yanapochimbwa madini ya Ruby
katika eneo la Mundarara alipofika ili kusikiliza mgogoro uliopo baina
ya wawekezaji wanaofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
![]() |
Mwekezaji
wa mgodi wa madini ya Ruby wa kampuni ya Mundarara Mine, akimwonesha Waziri wa
Madini Angellah Kairuki Seal inayotumiwa mgodini hapo kufunga eneo
yanapohifadhiwa madini ya Ruby baada ya uzalishaji.
![]() |
Mwekezaji wa mgodi wa
Mundarara Mine (kushoto) akiwaongoza Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kulia)
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea eneo la mgodi huo ili
kuangalia shughuli za uchimbaji namna inavtotekelezwa mgodini hapo.
![]() |
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki asalimiana na baadhi ya kina mama wa Kijiji cha
Mundarara mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho ili kuzungumza na
wananchi. Wanaofuatilia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati kulia)
na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe.
![]() |
Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Mundarara waliofika katika mkutano wa hadhara
kumsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika
machimbo ya Ruby yaliyopo katika kijiji hicho.
![]() |
Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Mundarara waliofika katika mkutano wa hadhara
kumsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika
machimbo ya Ruby yaliyopo katika kijiji hicho.
![]() |
Waziri wa Madini Angellah
Kairuki (katikati) akiwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mundarara baada ya kumpa
zawadi ya Vazi hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea machimbo ya Ruby
yanayochmbwa katika kijiji hicho pamoja na kuzungumza na wananchi. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
No comments:
Post a Comment