Greyson
Mwase na Asteria Muhozya, Morogoro
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki amesema kuwa viongozi pamoja na maafisa waandamizi
walioteuliwa kufanya kazi katika Tume ya Madini teuzi zao zinaweza kutenguliwa
iwapo watafanya kazi kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Waziri
Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 06 Agosti, 2018 wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya kazi kwa viongozi na maafisa waandamizi wa Tume ya Madini iliyofanyika mjini Morogoro na kuhudhuriwa na
watendaji na watumishi kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt.
delardus Kilangi.
Alisema
kuwa, Serikali imewateua kufanya kufanya kazi na Tume ya Madini huku ikiwa na matarajio makubwa ikiwa ni
pamoja na kuondoa kabisa urasimu kwenye utoaji wa leseni kwa kuhakikisha kuwa
wanatoa leseni kwa wakati, kutatua mogogoro ya wachimbaji wadogo na kuwa
wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini.
Aidha,
Waziri Kairuki aliongeza kuwa watendaji wapya wanatakiwa kuwa makini kwenye
zoezi zima la utoaji wa leseni kwa kuhakikisha kuwa wanahakiki historia za
waombaji wa leseni kwenye uchimbaji madini kabla ya kutoa leseni mpya.
“Ni
vyema mkahakikisha kuwa mnafahamu kwa kina historia za waombaji wa leseni za
madini hususan kwenye mapato na matumizi kwa mwaka, ulipiaji wa leseni,
ushiriki katika utoaji wa huduma za jamii, uzingatiaji wa kanuni za uhifadhi na
mazingira na kuwapatia leseni waombaji
wale tu watakaokidhi vigezo,” alisisitiza Waziri Kairuki.
Katika
hatua nyingine,Waziri Kairuki alitoa onyo kwa watumishi watakaothubutu kuhujumu
mfumo wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao ujulikanao kama online
mining cadastre transactional portal na kuongeza kuwa Wizara haitasita
kuwachukulia hatua za kisheria watakaohujumu mfumo.
Waziri
Kairuki aliwataka maafisa madini wa mikoa kuhakikisha wanaainisha maeneo kwa
ajili ya wachimbaji wadogo wa madini na kumpatia taarifa mapema na kuhakikisha
wanafanya mikutano ya mara kwa mara na wachimbaji wadogo ili kubaini changamoto
zao.
Awali
akielezea mafunzo hayo, Waziri Kairuki alisema mafunzo hayo ya siku sita
yatalenga kutoa elimu kuhusu historia ya mabadiliko ya sheria ya madini, sheria
ya madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017, muundo wa tume ya
madini na mawasiliano ya ndani na nje ya tume.
Aliendelea
kueleza maeneo mengine kuwa ni pamoja na muundo na mfumo wa mawasiliano wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), taratibu za ofisi na makusanyo
na maduhuli ya Serikali kwa njia ya kieletroniki (GEPG), usimamizi na utunzaji
wa mali za umma, taratibu za utoaji wa leseni za shughuli za madini na
ushirikishwaji wa wananchi/wazawa katika shughuli za madini.
Maeneo
mengine ni pamoja na ukaguzi wa madini na biashara, utatuzi wa migogoro katika
sekta ya madini, taratibu za uwasilishaji wa taarifa makao makuu ya Tume na
kwenye mamlaka nyingine zinazohusika, utunzaji wa siri katika utumishi wa umma,
masuala ya utawala na rasilimaliwatu, sheria, kanuni na taratibu za fedha,
usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa ndani, maadili katika utumishi wa umma na
mfumo wa uwazi wa upimaji utendaji kazi (OPRAS)
Alisema
kuwa kwa kuwa tume imepata watumishi wa
kutosha inatakiwa kuunda kamati mbalimbali za kisheria na kitendaji kama vile
kamati ya maadili, kamati ya ukaguzi, kamati ya ajira za kigeni na baraza la
wafanyakazi ili kuifanya tume iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Naye
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza katika mafunzo hayo alimshukuru
Waziri Kairuki kwa uteuzi wa watendaji wapya wa Tume ya Madini na kuwataka
washiriki wa mafunzo hayo kuyafanyia kazi yote watakayojifunza.
Wakati
huohuo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi alisema kuwa
mabadiliko ya sheria ya madini yaliyofanyika Tanzania ni hatua ya ushujaa na
kuongeza kuwa mataifa mengine yameanza kujifunza.
Alisema
kutokana na muhimu wa Sekta ya Madini kwenye mchango wa ukuaji wa uchumi wa
nchi ameamua kufika mwenyewe kuja kutoa mafunzo kwa viongozi na maafisa
waandamizi wa Tume ya Madini ili waweze kusimamia ipasavyo sekta hiyo kwa
kutumia sheria na kanuni za madini.
Sehemu
ya washiriki wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki (hayupo pichani) kwenye ufunguzi huo.
|
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko (kushoto) kwenye mafunzo hayo.
|
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya (kushoto) akibadilishana
mawazo na sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
|
Kaimu
Mhasibu Mkuu wa Tume ya Madini, Avodia Lukonge (kushoto) akibadilishana mawazo
na Mkaguzi wa Ndani kutoka Tume ya
Madini, Happiness Shirima kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa mafunzo hayo.
|
No comments:
Post a Comment