Na
Zuena Msuya, Kilimanjaro
Serikali imewataka Watanzania kuepuka migogoro katika maeno ya migodi hasa
inayomilikiwa Kwa ubia na wawekezaji wazawa ili kuondoa taswira mbaya kwa wawekezaji
kutoka Matifa mengine yanayokuja nchini kwa lengo la kuwekeza badala yake
waungane kuweka mazingira mazuri na
rafiki ya kuvutia wawekezaji hao kuwekeza nchini.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa ziara
yake mkoani Kilimanjaro alipotembelea
mgodi wa Madini wa Mega unaochimba madini ya shaba .( Mega Copper Company) uliopo
katika Kijiji cha Chang`ombe wilayani Mwanga
Mkoani Kilimanjaro, Kwan lengo la kumaliza mgogoro uliopo katika mgodi
huo unachimba na kuchenjua madini ya Shaba.
Mgodi huo wa madini ya Shaba unaomilikiwa na Watanzania
umekuwa katika migogoro ya kutoelewana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka
10 sasa, Licha kumepiga hatau katika uchenjuaji
wa shaba na kwamba hausafirishi madini ghafi nje ya nchi kama serikali ilivyoagiza.
Kwa mantiki hiyo, Biteko alisisitiza kuwa migogoro
haipaswi kupewa nafasi na inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania na kuleta
taswira mbaya ya Uwekezaji Tanzania katika Mataifa mengine Duniani Kwani kusengskuwa
na mgogoro katika mgodi huo wangekuwa wamepiga hatua zaidi kwa manufaa yao na Taifa
kwa jumla.
Biteko
alisema “migogoro miongoni ya wabia hasa wazawa haipaswi kufumbiwa macho
na mtu yeyote Yule, ambapo alishauri kuwa kama watu, au kikundi wameingia
makubaliano ya pamoja katika kuendeleza mgodi au jambo fulani basi, makubaliano hayo yapelekwe Wizara ya
madini au katika mamlaka husika yasajiliwe
kuepusha migogoro.
Aidha aliweka wazi kuwa kutokana na mgogoro, Serikali
imetoa Miezi 3 kwa mgodi huo kumaliza tofauti zao na kuendelea na shughuli za
uzalishaji, na endapo watashindwa kufanya hivyo, itawaandikia hati ya makosa na
kisha kuwanyang'a mgodi huo na kuwapa watu wengine.
“Ninyi wote ni Watanzania tena ni ndugu kwa nini
mnagombana? , Mnakuja kuwa Sheria ya madini inaruhusu kuwafungulia hati ya
mashitaka na kuwafutia leseni endapo mgogoro huo hautakwisha na utakuwa na viashiria vya uvunjivu wa amani na Mkishindwa
kuumaliza ndani ya muda uliotolewa Serikali unaingia Kati na kufanya maamuzi, nawakumbusha
watanzania wote hasa wanaoishi
katika maeneo karibu na migodi kuepuka migogoro ili sekta ya mdini iendeleee
kuimarika” alisisitiza Naibu waziri Biteko.
Vilevile alitoa wito kwa wanatanzania wenye uwezo wa kuongeza
thamani ya madini wafanye hivyo ili
kuongeza pato la taifa na mwananchi mmoja mmoja
kuliko kusafirisha madini ghafi nje ya nchi kwa kuwa faida kubwa zinapata nchi
zinazo nunua madini ghafi hayo na kuyaongeza thamani.
Kwa mujibu wa Naibu waziri Biteko mgogoro ulipo katika mgodi huo kati ya wabia Watanzania wawili ambao kila mmoja
alikuwa na mbao wake kutoka nje, ambao waliingia makubaliano
ya kuanzisha mradi huo ndani ya miezi sita, baadae Kuliitokea kutoelewana na kUsababisha mmoja kati
yao kuanza uzalishaji kabla ya
kumshirikisha mwenzie.
Mmoja wa wabia hao ni Ally Nyanza kutoka ambaye alisema kuwa mgodi huo una ukubwa wa heka 25,
ambapo kwa sasa wapo kwenye majaribio ya kuchimba na kuchenjua
shaba Ambapo wanauwezo wa kuzalisha tani 8-10 za shaba kwa siku.
Alisema Bado wanaendelea na tafiti huku wakiendelea
na uzalishaji, soko kubwa la shaba hiyo
liko nchini China na kutokana na
tafiti hizo wamegundua eneo hilo lina
chokaa ambayo hutumika kwenye uzalishaji wa saruji.
Nyanza alismea changamoto kubwa ilikuwa na mgogoro
kati yao na uliosabababisha kusimamisha uzalishaji kwa muda mrefu, kwa sasa wanafuata
maelekezo ya Naibu waziri kupata muafaka wa kufanya kazi pamoja.
Naye Nassib
Mfinanga alisema wamemeridhika na maamuzi ya Naibu Waziri wa
Madini na kwamba watakaa kama familia ili tusonge mbele kwani mgogoro huo umekuwa
ukituchelewesha na kutupa hofu kuwekeza bila kuwa na usalama, jambo hili
lilikuwa ngumu kwetu.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aaron Mbogho alisema
uwepo wa mgodi huo ni chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo tunasuburi
wameanza uzalishaji pamoja wazingatie sheriana kanuni za wizara serikali bado inatamani kuona watoka kwenye
uongezajiwathani ya shaba 90% hadi kufikia 100%.
![]() |
Naibu Waziri wa madini, Dotto Biteko, akizungumza na akina
mama wanaofanya kazi katika mgodi wa shaba wa Mega.
![]() |
Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko (kulia) akipita
katikati ya Mbale za shaba zilizoandaliwa tayari kwa kuchenjuliwa.
![]() |
Sehemu ya mtambo unaotumika Kuchenjua shaba.
No comments:
Post a Comment