Na
Zuena Msuya, Tanga
Serikali imempa muda wa wiki moja nwekezaji mmiliki wa kampuni ya Amazon Trading
(T)Company Limited Abdi Hozza kuhakikisha anailipa serikali kodi ya pango ya uwekezaji
kiasi cha dola za Marekani 70,020 sawa
na zaidi ya shilingi milioni 140 za kitanzania
anazodaiwa tangu mwaka 2011 katika machimbo ya Kalalani eneo la Umba
wilayani Korogwe kutokana na leseni nane za uchimbaji wa madini
kuanzialeseni namba (102-109/2001)
anazomiliki.
Sambamba na hilo imeiagiza serikali ya wilaya ya
Korogwe kuhakikisha inatenga maeneo ya
wachimbaji wadogowadogo wa madini ili kuepusha migogoro iliyodumu kwa muda
mrefu hali ambayo imeleta hali ya chuki baina ya mwekezaji na wananchi.
Waziri Biteko alitoa agizo hilo alipotembelea
katika machimbo hayo juzi Jumamosi katika vijiji vya Kigwasi na Kalalani kata
ya Kalalani wilayani humo.
Biteko alimtaka ndani ya wiki moja mwekezaji huyo kulipa
kodi hiyo ya pango anayodaiwa na serikali na amewataka wananchi kutoa ushirikiano
katika kuwabaini wageni na watu wanaonunua madini kwa njia za panya.
“Haiwezekani tangu madini yaanze kuchimbwa katika machimbo
haya serikali haijapata kodi kutokana na mgodi huu tunakuta sifuri nimewaambia wailipe
haraka nataka nikifika Dodoma kuna commitment statement mnalipa lini” alisema.
Aliongeza “Na
yule anayedhani atakuja Kalalani kununua
madini kwa njia ya panya muda huo umekwisha,na tumekwenda kwenye mto tumekuta
mnachimba madini,sheria inakataza kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji naomba
kuanzia sasa mkaondoe vifaa vyenu kule mtoni”.
Aidha Waziri Biteko, aliongeza kuwa eneo hilo la Kalalani
lina leseni za wachimbaji wadogo wa madini ya vito zipatazo 400 lakini leseni
zilizohai na zinaendelea kufanya kazi ya uchimbaji ni 70 tu kati ya hizo.
Awali diwani wa kata hiyo Amati Ngerera alimueleza
naibu waziri kuwa mwekezaji huyo(Amazon)hana mahusiano mazuri na wa wanakijiji
pamoja na wachimbaji wadogowadogo wa hapo kutokana baada ya kupewa leseni na
serikali kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo
alilitelekeza kwa muda mrefu bila ya
kuendeleza shughuli zozote na wananchi wengi ambao shughuli zao kubwa ni
uchimbaji waliokuwa wakiingia eneo hilo walifanyiwa vitendo vya visivyokuwa vya
kibinadamu ikiwemo kupigwa risasi,kubakwa na askari aliowaweka kulinda eneo
hilo.
Diwani huyo alikwenda mbali zaidi kuwa mwekezaji
huyo huwa anatumia eneo hilo kama dhamana ya kukopa fedha kutoka kwenye taasisi
za fedha na alimpa mwenzake anaitwa Najim
kuendesha mgodi huo kinyemela bila ya serikali kuwa na taarifa.
“Huyu mwekezaji leseni yake ilikwisha tangu mwaka
2001,wananchi wakaomba leseni ya uchimbaji na yeye akaomba ,lakini baadae akaingia mkataba na mfanyabiashara anayeitwa
Najim halafu yeye akajitoa kabisa na huyo Najim hachimbi bali anafanya shughuli
zake za biashara ya utalii na huyu Amazon anatumia eneo hili kukopea fedha
kwenye taasisi za fedha ”alisema.
Aliongeza “Serikali ya kijiji ilifanya mapendekezo
matatu na kuyapeleka katika baraza la madiwani na baadae tukayandika kuyaleta
katika ofisi yako,mapendekezo haoy ni eneo hilo litafutwe mwekezaji mwenye sifa
ya uwekezaji,nyumba zilizopo eneo la mgodi
zirudishwe serikalini ambazo waasisi wake ni STAMICO na wananchi
wakatiwe eneo ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi za uchimbaji”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwasi, Loronyotu
Lakaney alimueleza Naibu Waziri kuwa mbali na mgodi huo kutelekezwa na
mwekezaji huyo pia madini yanatorosha kwa njia za panya na kuuzwa Voi nchini Kenya.
“Mheshimiwa Naibu waziri mbali na mgogoro huo pia
wachimbaji wengi wadogowadogo wakishapata madini wanakwenda kuyauza Voi mpakani
mwa Kenya na Tanzania upande wa hapa Tanga kutokana hakuna udhibiti na hakuna minada ya madini inayoendeshwa kama
serikali ilivyoagiza”alisema.
Naye mwekezaji huyo alimueleza Naibu waziri kuwa
alichelewa kulipa hiyo kodi kutokana Kutokupewa taarifa yoyote ya kuendeleza
mgodi wala kudaiwa kodi.
“Mheshimiwa Naibu waziri mimi ni kweli kwa muda
mrefu sijapaendeleza hapa baada ya leseni yangu kwisha mwaka 2011 sijapewa
leseni nyingine wala sijapata hiyo barua ya kulipa hiyo kodi ya pango”alisema.
Taarifa ya ofisi ya Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga amabayo gazeti hili inayo
nakala yake ilishapendekeza kwa kamishna
wa madini leseni hizo nane za mwekezaji ziandikiwe hati ya makosa(default
notice) na hatimaye zifutwe kwa mujibu wa sheria ya madini mwaka 2010,lakini
kwenye mfumo wa flexicadastre leseni hizo zinaonesha zipo hai(active in
default) ingawa zilishaisha muda wake tangu Septemba 30,2011.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko, akikagua Mabaki ya mgodi wa Amazon,ambao umesitisha uchimbaji kwa miaka mingi kutokana na Matatizo mbalimbali. |
Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko (aliyesimama) akizungumza
na wachimbaji wadogo wa eneo la Kilalani, baada ya kutembelea eneo hilo.
|
No comments:
Post a Comment