Monday, July 9, 2018

Wizara za Nishati, Madini zaendelea kuelimisha kwenye Maonehso ya Sabasaba

Sehemu ya wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Environmental Foundation for Tanzania, Rehema Mwambenja, (kulia) akielezea matumizi ya nishati mbadala kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).


Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Madini, Assa Mwakilembe (kulia) akielezea bidhaa zinazotengenezwa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC) kwenye maonesho hayo.

Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Madini, Assa Mwakilembe (kushoto) akionesha bidhaa zinazotengenezwa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC) kwenye maonesho hayo.

Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata huduma kwenye banda la Wizaya ya Madini kwenye maonesho hayo.

Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi  ya Shirika la Umeme  Tanzania (Tanesco) Dk. Kyaruzi  (kulia) akipata maelezo ya majukumu ya Wizara ya Madini kutoka kwa Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Madini, Assa Mwakilembe (kushoto).

Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi  ya Shirika la Umeme  Tanzania (Tanesco) Dk. Kyaruzi  akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC).

No comments:

Post a Comment