Na
Samwel Mtuwa, Dodoma
Mradi wa Usimamizi
Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ulio chini ya Wizara ya Madini,
unatarajia kujenga jengo kubwa la kuingiza kiasi cha Wanafunzi 200 kwa wakati mmoja katika Chuo Cha Madini
Dodoma.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki na
Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati akitolea ufafanuzi changamoto
zilizowasilishwa na Serikali ya Chuo hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Madini chuoni hapo.
Alisema, ujenzi huo
unatarajia kuanza mwezi Julai mwaka huu
na kuongeza kuwa wizara kupitia
wadau wake wa maendeleo itajenga viwanja vya michezo chini ya usimamizi wa
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Kwa upande wake, Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, Chuo Elia Mwita alimwomba Waziri Kairuki kuwakutanisha na
wadau wa sekta ya madini nchini ili kuwawezesha kupata fursa ya kuonesha ujuzi
waliopata kutoka katika Chuo hicho.
Mbali na ombi hilo,
Mwita aliwasilisha maombi mbalimbali ya wanafunzi ikiwemo kutumiwa kama mabolozi pindi
wanapomaliza mafunzo yao, kupatiwa fursa za udhamini wa masomo ya juu kupitia
wizara, kuwapatia fedha za kujikimu
wakati wa mafunzo na kuingizwa katika Huduma ya Afya kupitia Bima ya Afya.
Sambamba na kufanya
mikutano ya uongozi wa wanafunzi, pia Waziri
Kairuki alitembelea maonesho ya kazi za wanafunzi, kugawa zawadi kwa timu
zilizoshinda katika michezo mbalimbali iliyofanyika, ambapo katika siku hiyo MRI
iliitambua siku hiyo kama Siku ya Madini.
Pia, Waziri Kairuki
alipokea Muhtasari wa taarifa ya chuo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Bw. Vincent
Pazzia pamoja na risala kutoka kwa Rais wa Serikali ya Chuo hicho, Elia Mwita.
Katika maadhimisho
hayo, Waziri Kairuki aliambatana na Naibu Waziri Stanslaus Nyongo, Viongozi wa
Wizara na Taasisi.
Matukio
mbalimbali yakimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki pamoja na Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakipata maelezo kuhusu namna mashine na
vifaa mbalimbali vya utafiti, uchenjuaji , na utenganishi wa madini pamoja na
uchimbaji bora wa madini kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira kutoka kwa
wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma ikiwa sehemu ya kazi mbalimbali
zinazofanywa na wanafunzi hapo chuoni.

Waziri
wa Madini akizungumza na wanafunzi wa Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) katika
ukumbi wa chuo hicho. Waziri Kairuki
alitembelea chuo hicho ikiwa ni moja ya ahadi aliyoitoa alipokitembelea Chuo
hicho awali.

|
No comments:
Post a Comment