Monday, July 9, 2018

Naibu Waziri Biteko atembelea mabanda ya Wizara za Madini na ishati kwenye Maonesho ya Sabasaba

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akiangalia vipeperushi kwenye Banda la Wizara ya Madini mara alipotembelea mabanda ya  Wizara za Madini na Nishati kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mjiolojia na Mkufunzi katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Ester Njiwa (kulia) akielezea matumizi ya mashine maalum zinazobeba madini ya vito wakati wa ukataji  kwa Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (kushoto)kwenye maonesho hayo.

Mhandisi Mitambo katika Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC),  Amani Christopher (katikati) akielezea matumizi ya mashine ya kutafiti jotoardhi kwa Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko kwenye maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akiangalia vipeperushi kwenye Banda la Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Gesi na Mafuta (TEITI) kwenye maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akisaini kitabu cha wageni kwenye Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwenye maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wa Wizara ya Madini kwenye maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment