Na Greyson Mwase
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wanaoendesha
shughuli za uchimbaji madini kwa njia ya ujanja ikiwa ni pamoja na kukwepa
kulipa kodi serikalini, kutafuta kazi nyingine kwani Serikali ya Awamu ya Tano
kupitia Wizara ya Madini imejipanga kudhiti biashara haramu ya madini.
Naibu
Waziri Biteko aliyasema hayo leo tarehe 21 Julai, 2018 kwenye mkutano wake na
wazalishaji wa chumvi, wachimbaji madini ya jasi pamoja na wawakilishi kutoka
kampuni ya saruji ya Dangote uliofanyika mjini Mtwara wenye lengo la kufuatilia
maelekezo aliyoyatoa katika kikao kilichofanyika mapema tarehe 19 Januari,
2018, kubaini changamoto kwenye shughuli za madini pamoja na kuzitatua.
Alisema
kuwa Wizara ya Madini imejipanga katika kudhibiti mianya yote ya ukwepaji kodi,
utoroshaji wa madini na rushwa ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na
mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akielezea
mikakati ya Serikali katika kuboresha shughuli za wachimbaji wa madini ya
chumvi Biteko alisema kuwa, Serikali imeondoa kodi zote zisizo za lazima ili
wachimbaji wadogo wapate faida zaidi na kulipa kodi stahiki serikalini.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliagiza wachimbaji madini hao kuhakikisha
wanalipa kodi stahiki ya madini mara baada ya kufanyika kwa mauzo kwenye kituo
cha mwisho (gross value) badala ya mauzo ya hapo hapo mgodini (net
back value).
“Sheria
ya Madini ya Mwaka 2010 kifungu cha 87 (6) kinaeleza kuwa kodi ya madini
itakokotolewa baada ya bei ya mwisho nje ya nchi kule yanapouzwa madini hayo na
si mgodini,” alieleza Biteko
Aliendela
kusema kuwa wakati wa kufanya biashara ya madini kwa ufanisi ni sasa kwani
hakuna urasimu na ujanja serikalini, hivyo kupelekea leseni za madini kutolewa
kwa wakati na kusisitiza kuwa kinachohitajika kwa wachimbaji wadogo ni kufuata
sheria na kanuni za uchimbaji madini.
Wakati
huo huo wachimbaji wadogo wa madini katika mikoa ya Lindi na Mtwara
walimpongeza Naibu Waziri Biteko kwa kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili
kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 kwa muda mfupi tu wa miezi sita tu.
“Mheshimiwa
Naibu Waziri tunashukuru mno kwani tangu ulipokutana na sisi mapema Januari 19,
mwaka huu mjini Mtwara na kutoa maelekezo kwa watendaji na kufuatilia maelekezo
yako, changamoto zote zimeisha ndani ya miezi sita, tuaendelea kuunga mkono
juhudi zako za kuboresha sekta ya madini kupitia wachimbaji wadogo,” alisema
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Lindi (LIREMA), Peter Ludovick
kupitia taarifa yake kwa Naibu Waziri Biteko.
Akielezea
pongezi hizo, Biteko alisema yeye hastahili pongezi hizo bali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kuwa yeye ndiye aliyeelekeza Wizara ya Madini
kuwaondolea wachimbaji kero.
Aliendelea
kusema kuwa anayestahili kupongezwa ni
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambaye
ndiye msimamizi mkuu wa Wizara ya Madini pamoja na Wizara ya Fedha kwa
kukubali kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fedha na kusisitiza kuwa hao
ndio wanaostahili pongezi na sio yeye.
Wakati
huohuo, Biteko alikutana na watumishi wa Ofisi ya Madini Mtwara na kuwataka
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku
akiahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji kazi.
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa (kulia) kabla ya kuanza ziara ya kikazi
katika mkoa Mtwara tarehe 21 Julai, 2018.
Naibu
Waziri wa Madini, Dotto Biteko (kushoto) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya
Madini Mtwara.
|
No comments:
Post a Comment