Na Asteria Muhozya, Dodoma
Waziri
wa Madini Angellah Kairuki ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuisaidia
wizara iweze kubaini maeneo maalum ya kuzingatia yatakayowezesha kuongeza
mchango wa Sekta katika Pato la Taifa.
Aliongeza
kuwa, ushauri utakaotolewa na NBS
utaisaidia wizara kujipanga zaidi kuhusu namna ya kutumia fursa zilizopo katika
sekta husika na sekta nyingine ili kuhakikisha kuwa pato la Sekta linaongezeka.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo tarehe 23 Julai, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma,
wakati wa kikao kati ya Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake ambapo Kaimu
Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa, aliwasilisha mada
kuhusu Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa.
Kikao
hicho kinafuatia maelekezo ya Waziri Kairuki aliyoyatoa kuhusu wizara kukutana
na NBS ili isaidie kuona ni namna gani wizara itaongeza mchango wake katika
pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 ifikapo
mwaka 2025.
Pia,
Waziri Kairuki aliwataka Watendaji wa wizara na taasisi husuan Tume ya Madini
kupitia kila vifungu vya Sheria ya Madini na kuhakikisha kuwa vinatekelezwa
kikamilifu.
Aidha,
Waziri Kairuki alimshukuru mtaalam huyo na kuikaribisha ofisi ya NBS kuendelea
kuishauri wizara kuhusu masuala ya takwimu kwa lengo la kuipeleka mbele sekta
ya madini.
Wakati
akiwasilisha mada, Musolwa aliishauri wizara kusimamia vizuri mianya ya mapato
yatokanayo na madini pamoja na kuongeza juhudi katika kuhakikisha inapata
taarifa za kutosha hususan katika madini ya ujenzi.
Pia,
aliishauri wizara kuhusu kufanya tafiti za madini katika maeneo mbalimbali ya
nchi jambo ambalo litaiwezesha kupata taarifa zitakazosaidia katika ukusanyaji
wa mapato stahiki kutokana na shughuli za madini zinazofanyika katika
sekta ikiwemo zile zinazokwenda sambamba na sekta ya madini.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alimshukuru mtoa mada kutokana
na elimu ya takwimu aliyoitoa na kuahidi kuufanyia kazi ushauri alioutoa.
Pia,
ameitaka NBS kuendelea kutoa ushauri wa mara kwa mara wizara lengo
likiwa ni kuhakikisha sekta ya madini inachangia zaidi katika pato la taifa.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki, akifuatilia
jambo wakati Kaimu Mkurugenzi Takwimu za
Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada Mchango wa Shughuli za
Madini katila Pato la Taifa.Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Kaimu Mkurugenzi Takwimu za
Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada ya Mchango wa Shughuli za
Madini katila Pato la Taifa kwaWaziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo
pichani) na Menejimenti ya Wizara pamoja na
watumishi kutoka Taasisi zake wanaofuatilia.
Kaimu Mkurugenzi Takwimu za
Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada ya Mchango wa Shughuli za
Madini katila Pato la Taifa kwaWaziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo
pichani) na Menejimenti ya Wizara pamoja na
watumishi kutoka Taasisi zake wanaofuatilia.
No comments:
Post a Comment