Na
Zuena Msuya, Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kasim Majaliwa amezindua Maabara ya kisasa ya utambuzi wa uasili wa madini iliyojengwa
katika Kituo cha Madini na Jiosayansi Afrika kilichopo eneo la Kunduchi Mtongani,
jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kuzindua maabara hiyo,
Juni 8, 2018, Waziri Mkuu Majaliwa alisema maabara hiyo itakuwa na uwezo wa kutambua
asili ya madini yote yanayochimbwa NA kupatikana duniani.
Vile vile italinda madini ya kila nchi husika hasa
kwa nchi za Afrika na kumaliza kabisa tatizo la utoroshwaji wa madini ya aina
yoyote kutoka nchi moja kwenda nyingine.
“Maabara hiyo itakuwa na uwezo wa kutambua mahali
ambapo madini hayo yamechimbwa au yanapatikana, na haitakuwa rahisi kwa mtu yeyote kufanya udanganyifu wa
kutorosha madini hayo kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwani kila nchi
yatakapokuwa yatakapopelekwa madini hayo vipimo vitaonyesha asili yanapotoka
madini hayo”, alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Alifafanua zaidi kuwa Maabara hiyo pia inauwezo
mkubwa wa kupima na kutambua asili ya madini Bati( Tin),Tantalam na Tantalite,
yanapochimbwa na yanapotoka, jambo ambapo litaondoka tatizo la kubaini kuwa
madini hayo lilipo sasa kwa nchi za afrika zinazochimba madini hayo ikiwemo
Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemograsia ya Congo.
Hivyo amezishauri nchi za Afrika kutumia maadara
hiyo ambayo kwa sasa inapatikana Tanzania pekee kwa nchi za afrika na niya pili
kujengwa duniani, ili nchi hizo ziweze kufahamu madini yake halisi
yanayopatikana katika nchi husika.
“ kwa mfano hapa Tanzania tunawachimbaji wadogo
wengi sana wanachimba madini lakini wengi wao wanashindwa kutambua ni madini
gani wanachimba, pia tunapokamata madini mipakani wengi husema madini hayo
yanatoka nchi jirani na hivyo tunakosa uthibitisho, sasa maabara hii ni
muarobaini wa kutatua changamoto zote hizi, na ni imani yangu kubwa italeta
manufaa makubwa katika sekta ya madini”, alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Aliweka wazi kuwa kuwepo kwa maabara hiyo Afrika kutamaliza
kabisa tatizo la uotoshwaji wa madini kutoka sehemu moja kwenda nyinge na
kuondoa udanganyifu na unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu kwa kusema ukweli
kuhusu mahali yanapopatikana madini husika.
Maabara hiyo inauwezo mkubwa wa kupima madini na
kutumia muda mfupi katika kutambua uhalisia wa madini.
Sambamba na hilo, Waziri Mkuu, Majaliwa alisema
maabara hiyo ya kisasa itarahisisha biashara ya madini kwa kila nchi husika na
kuleta manufaa zaidi kwa taifa na wake.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa( kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,(kulia) mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kituo cha Madini na Jiosayansi Afrika alipowasili kuzindua Maabara ya kwanza ya kisasa Afrika na ya pili duniani ya kutambua uasili wa madini. |
No comments:
Post a Comment