Na Rhoda James, Dar
es Salaam
Makatibu Wakuu kutoka
nchi Wanachama wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) wameshiriki
katika kikao cha 21 cha Kituo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Akifungua rasmi kikao
hicho kilichofanyika tarehe 6-7 Juni, 2018, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini
Tanzania, Prof. Simon Msanjila ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza, alisema
kuwa, kituo hicho hakina budi kuweka jitihada katika kuhamasisha nchi nyingine za Afrika ambazo bado hazijajiunga ili
ziweze kujiunga na kituo hicho.
Pia, alieleza kuhusu
umuhimu wa kituo kuendelea kuweka msisito kwa nchi wanachama kulipa ada za
uanachama kwa wakati na kuhakikisha kuwa kinatekeleza majukumu yake kwa ubora
uliokusudiwa.
Akichangi mada, Prof.
Msajila alizungumzia kuhusu suala la upatikanaji wa eneo la ujenzi wa vinu vya
kuchenjua na kuongeza thamani madini na kushauri kuhusu kuzingatia suala ya
uhifadhi wa mazingira.
Pia, Profesa Msajila
alikitaarifu kikao hicho kuhusu ushiriki wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amon Maganga pamoja na Wataalam mbalimbali
kutoka taasisi hizo katika Mkutano wa 38
wa Wakuu wa nchi wanachama utakaofanyika tarehe 8 Juni, 2018.
“Nimeeleza kuhusu ushiriki wa Watendaji hao
kwa lengo la kujadili suala la kufanya biashara na kituo cha AMGC kwa kuwa vipo
vifaa ambavyo kituo chetu kinaweza kuvizalisha kwa matumizi ya taasisi za REA
na TANESCO,” alisema Prof. Msanjila.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Kikao hicho Dkt. Kojo Busia alisema kuwa, asilimia 75 ya madini
ya Coltan hupita katika Bandari ya
Dar es Salaam Tanzania kuelekea nchi jirani ukilinganisha na asilimia 25 ambayo
hupita Mombasa nchini Kenya na kueleza umuhimu kituo hicho kuboreshwa ili kutoa
huduma bora zaidi.
Pia, Dkt. Busia
alisisitiza suala la kituo cha AMGC kuona namna bora ya kuungana na Taasisi ya
African Minerals Development (AMDC) ili
kuwa chombo kimoja ambalo litapelekea kuongeza ufanisi wa kituo hicho.
Nchi wanachama wa
kituo cha AMGC ni Tanzania, Angola, Msumbiji, Sudani Kaskazini, Ethiopia,
Uganda, Kenya, Comoro na Burundi.
Wajumbe mbalimbali waliohudhuria kikao cha 21 cha Makatibu wakuu kilichofanyika katika Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) Kunduchi, jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC), Assa Mwakilembe akichangia mada katika kikao hicho. Kulia kulia kwake Mjumbe kutoka nchi ya Uganda. |
Wajumbe mbalimbali waliohudhuria kikao cha 21 cha Makatibu wakuu kilichofanyika katika Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) Kunduchi, jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment