Na
Samwel Mtuwa, Dodoma
Wizara ya Madini
imefanya Semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
pamoja na Kamati ndogo ya Sheria ya Bunge juu ya Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
Akizungumza katika
semina hiyo, Katibu wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Tanzania, Casmir Kyuki,
alieleza kuwa, semina hiyo imelenga kuwaelemisha Wabunge kuhusu
Sheria Mpya ya Madini ya mwaka
2017 baada ya kufanyika Marekebisho kadhaa katika Sheria ya Madini ya Mwaka
2010.
Aidha, pamoja na
kupata elimu kuhusu sheria hiyo, wajumbe
wa kamati hizo walipata fursa ya kuelimishwa
kuhusu Kanuni Saba za Sheria ya Madini ambazo ni Kanuni ya Umiliki
wa madini; Kanuni ya Biashara ya madini; Kanuni ya uendeshaji wa wananchi Kanuni
ya madini ya mionzi.
Kanuni nyingine ni pamoja na Kanuni ya uongezaji
thamani madini na Kanuni ya utafiti wa kijiolojia na Kanuni ya hifadhi ya ukaguzi wa hesabu na
kumbukumbu.
Kwa upande wake, Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Flurence Luoga aliwaeleza wabunge kuhusu sababu za maboresho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Sheria ilimpa mwekezaji uhuru mkubwa ndani ya sekta ya madini.
"Uhuru huo ni pamoja na uhuru wa kuchimba , kusafirisha , kufanya
uchenjuaji nje ya nchi, pamoja na kufanya tafiti bila kuwasilisha taarifa za kijiolojia na madini,"alieleza Luoga.
Akielezea juu ya
sababu za kuwepo kwa uhuru huo katika sekta ya madini kabla ya maboresho ya Sheria
ya 2018, Gavana Luoga alifafanua kuwa
suala hilo lilitokana na Sheria zilizokuwepo tangu enzi za Serikali ya kikoloni.
Semina hiyo
iliendeshwa na wabobezi wa masuala ya
sheria , fedha na madini ambapo walitoa mada mbalimbali kuanzia
historia ya mikataba ya kisheria ya kitaifa na kimataifa juu ya sekta ya
madini tangu enzi za serikali za kikoloni za Ujerumani na Uingereza.
Watoa mada Wakuu
katika semina hii walikuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti
Madini Tanzania (GST), Profesa Abdulakarim Mruma Profesa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Florence Luoga na Katibu wa Tume ya kurekebisha sheria
Tanzania Casmir Kyuki.
Semina ilifanyika
tarehe 19 Mei 2018, katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ndani ya ukumbi mdogo wa Pius Msekwa na
kuhudhuria na kutoka Vyama mbalimbali
vya siasa, Watendaji wa Wizara na Watalaam wa
Sheria na Madini kutoka wizara
ya Madini.
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
Baadhi ya
Wabunge na Watendaji wa Wizara
wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya
Madini ya Mwaka 2017.
|
No comments:
Post a Comment